WAZIRI NAGU ATEMBELEA KIWANDA KINACHOTOA AJIRA KWA WALEMAVU KUWAWEZESHA KIUCHUMI
Aliyeshika karatasi ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dr. Mary Michael Nagu akibainisha fursa mbalimbali za Uwekezaji zilizo Tanzania. Akihutubia Wafanyabiashara hao amewashauri kuchangamkia fursa mbalimbali katika sekta za kilimo, gesi, utalii, madini na ujenzi. Kongamano la Biashara limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji kwa kushirikiana na Taasisi ya Biashara ya Ubelgiji na Luxembourg.