WAZIRI NAGU ATEMBELEA KIWANDA KINACHOTENGENEZA MITAMBO YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO
Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Michael Nagu akimsikiliza
Meneja wa kiwanda cha kutengeza mitambo ya kutumika kwenye viwanda
vidogo vya bia, maziwa ya kawaida na maziwa ya soya. Mitambo hii ni kwa
ajili ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa nia ya kuwezesha watu
kiuchumi, kutoa ajira kwa vijana na kuongeza thamani mazao ya kilimo.
Serikali ya Ubelgiji inagharamia asilimia hamsini ya ununuzi wa mitambo
hiyo. Mhe Nagu ametembelea kiwanda hicho leo Ghent Ubelgiji.