BALOZI KAMALA APOKEA VIFAA VYA MCHEZO WA MPIRA KUTOKA CHAMA CHA MPIRA CHA UBELIGIJI
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati)
akiwa na Viongozi wa Chama cha Mpira cha Ubeligiji baada ya kupokea
vifaa vya mchezo wa mpira. Kulia ni Msaidizi wa Rais wa Chama cha Mpira
cha Ubeligiji Bwana Thomas Pereira na kushoto ni Bwana Frederic
Veraghame Meneja Mwendeshaji wa Chama cha Mpira cha Ubeligiji. Balozi
Kamala amepokea vifaa hivyo leo mjini Tubize Ubeligiji. Pamoja na mambo
mengine, Balozi Kamala amekubaliana na Viongozi hao kuandaa mpango wa
ushirikiano wa kuendeleza mchezo wa mpira kati ya Tanzania na Ubelgiji.