BALOZI KAMALA ATAMBUA MCHANGO WA TAASISI YA CUSHMAN NA WAKEFIELD ILIYOSAIDIA UJENZI WA SEKONDARI YA MIONO YA MKOANI PWANI
Balozi wa Tanzania Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya Ulaya Dr. Diodorus
Buberwa Kamala (kushoto) akimkabidhi cheti Bwana Boris Van Haare
Heijmeijer Meneja wa Ulaya wa taasisi ya Cushman na Wakefield cha
kutambua mchango wa taasisi hiyo wa kusaidia ujenzi wa Sekondari ya
Miono ya Mkoani Pwani. Taasisi hiyo imechangia Shilingi Bilioni 1.2 na
imehaidi kuongeza Shilingi Milioni Mia Mbili. Balozi Kamala ameishukuru
taasisi hiyo na ameiomba iendelee kusaidia shule hiyo.