IPTL YAIMWAGIA TASWA MILIONI 20 KUANDAA TUZO ZA WANAMICHEZO
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent
Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (kushoto) akikabidhi mfano
wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 20 kwa Mwenyekiti wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (wapili kulia) ikiwa ni
mchango wa IPTL kusaidia maandalizi ya Tuzo za wanamichezo bora nchini. Wanaoshuhudia
kutoka kushoto ni ni Makamu Mweyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko, Katibu Mkuu,
Amir Mhando na Mwanasheria na Mshauri Mkuu wa IPTL,Joseph Makandege na kulia ni Mjumbe wa TASWA, Rehure Richard Nyaulawa
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akizungumza na wanahabari baada ya kupokea fedha hizo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent
Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth akiwaeleza wanahabari furaha yake ya kuisaidia TASWA kitita hicho cha fedha kusaidia wanamichezo ambapo nae alikiri kuwa ni miongoni mwa wanamichezo na amewahi kuwa Mshindi wa tatu wa Mbio za Magari Afrika.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent
Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (katikati) akiwaongoza wanahabari kuangalia mitambo ya Kampuni hiyo ambayo inazalisha umeme. Kulia ni Katibu mkuu wa TASWA, Amir Mhando na Kushoto ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto.
Waandishi wa habari wakiingia kuangalia uzalishaji wa umeme katika mitambo ya IPTL.