Bukobawadau

KIFO CHA MAMA COLLETHA RWEYEMAMU

Ibada ya kumwombea marehemu Colletha Rweyemamu iliyofanyikia Jioni ya leo oct 22,2014 katika kanisa la Bugando Hosp, Jijini Mwanza muda mchache kabla ya safari kuelekea bukoba,tayari kwa SHUGHULI ya Mazishi zitakazofanyika siku ya Jumamosi Kijijini Kishoju -Nshamba Wilayani Muleba .
    
Pichani kulia anaonekana Ndugu Rady Rweyemamu ambaye ni mtoto wa marehemu,Kwa hivi sasa Msiba unaendelea Nyumbani Kwa Adv Rweyemamu mtaa wa Miembeni Bukoba
 
Muda mchache kabla ya kusafirisha mwili wa Marehemu Collettha,sehemu ya waombolezaji wakiwa wamefika Bugando kuwafariji wafiwa,kushoto anaonekana Ndg Azizi Kichwabuta rafiki wa familia.
Taarifa za awali zinasema kwa siku ya KESHO Alhamsi  kutakuwa na Misa maalum ya kumuombea Marehemu Colletha Rweyemamu itakayofamnyika  Nyumbani kwake Miembeni Bukobai majira ya saa kumi jioni.
BUKOBAWADAU BLOG tunatoa pole kwa familia ya Mzee wetu Adv. Rweyemamu kufuatia kifo cha  Mke wake Mpendwa COLLETHA RWEYEMAMU, tunatoa pole kwa watoto  wa Marehemu ndugu jamaa na marafiki.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau