Bukobawadau

MAINDA ...!''SASA NI MR & MRS JAMAL RASHID''

 Tusipo sema Dada Mainda  congratulations hakika tutakuwa tunakosa adabu, Si vyema kusema ni nini katufanyia na nini tumepata kutoka kwake, Tunachoweza kusema ni kitu kimoja tu; My Dear Lovery Sister  Mai wa Mainda biharusi  Mwanahawa Hongera sana.
Hongera sana Ndugu, hongera sana Mtoto wa Kitanga,hongera kwa Shemeji yetu Jamal, hongera kwako tena  Mwanapamoja Mwanahawa  mtoto wa Miembeni hakika ukipita anayekupenda mshikilie ,mshikilie mwenye tabia za kupendeza mshikilie, mwenye heshima kwa watu woteee, na mikono yote, usiachilieeeee Daima.
 Katika picha ya kumbukumbu na Dada Mpendwa Rukia Mawenya na Mmewe (kulia)
 Picha zote kwa hisani ya Jamal Kalumuna ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Shughuli nzima, kuma anavyo onekana pichani kushoto akimkaribisha sheikh Haruna Kichwabuta.
 Anafurahia Jambo Ndugu Mohamed Kassim na Bwana Shemeji pichani kulia
 Sheikh mkuu Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta (kushoto) akifungisha ndoa Bw.Jamal
 Bwana Harusi Jamal Rashid akimwaga Wino katika Cheti cha ndoa
Bwana harusi anapongezwa mara baada ya Kitendo kusaini Cheti cha Ndoa
 Cheti cha ndoa ndo kila kitu ndivyo anavyo fanya kusaini Cheti cha Ndoa yake Bi Mainda
 Shuhuda wa tukio zima Ndg Al Amin Abdul anasema;'Mwanamke ndoa'
 Sheikh wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta akitoa nasaha zake.
 Fursa kwa Bwana Jamal Rashid, kutanguliza Dua kabla ya kumfunua Mkewe.
Baba Mzazi wa Bi Mainda ,Mzee Kassim pichani kulia akikabidhi cheti cha Ndoa
Bi harusi wetu Bi Mainda katika picha ya pamoja na Dada zake wapendwa.
  Sasa ni Mr & Mrs Jamal  Rashid ,Bwana Jamal Yuleee...! 'anaondoka na mkewe Mainda'!!
Kwa ufupi hivi ndivyo mambo yalivyokuwa ,Ndugu  Mwinyi pichani ni kati ya mashuhuda.
 Sehemu ya Msafara wa Magari kutoka kwa Wadau walioshiriki kikamilifu katika shughuli hii.
 Bukobawadau Blog tunawapongeza  sana Mola awajalie na kuwaongoza katika maisha ya ndoa yao!!!

Next Post Previous Post
Bukobawadau