Bukobawadau

MDAU FIDEL 'BLONZO DA ONE' ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WATOTO YATIMA

Jana Octa 24 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwake Kijana mwenzetu Fidel maarufu kama 'Blonzo Da Öñè'  Mkazi wa Rwamishenye Mjini hapa.
Ndugu Fidel pichani aliamua Fidel Blonzo Da Öñè alivyo amua kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na watoto yatima wa kituo cha 'NUSURU  YATIMA' kilichopo Kashai Mjini hapa.
Mara baada ya kuwasili kituoni  hapo wanapokelewa na Mama ambaye ndiye Mlezi wa Kituo hicho Bi Mariam Mahya maarufu kwa jini la Nurudhiha pichani kulia.
 Anaonekana Bi Diana pichani
  Katika tukio hilo Mdau Fidel Blonzo Da Öñè aliongozana na Mkewe Bi Dyna pichani kushoto pamoja na marafiki zake wa karibu,pichani kulia ni Dj Slay mmoja wa marafiki.
 Katika hafla hiyo Ndugu Fidel na marafiki zake walijumuika na Watoto hao kwa kula ,kunywa  na kufurahi kwa pamoja kama wanavyo onekana sehemu ya kundi la watoto hao wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa sababu nyingi. katika kundi la yatima hawa baadhi yao wamefiwa na wazazi na wapo waliozaliwa wakiwa na upungu mwilini.
 Utaratibu kwa kila mtoto kupata zawadi zilizotoka kwa Mdau Mr. Fedel Blonzo Da One.
 So insipirational!!
Tunashuhudia Mtoto akijaribu kumuhudumia mtoto mwenzake hakika hii ni changamoto katika kundi hili maalum la Watoto yatima,wanaoishi katika mazingira hatarishi
 Ukosefu wa huduma za serikali kwa watoto hao,  kumewatia huruma wadau mbalimbali kuchukua hatua za kuanzisha vituo vya kulea watoto ili  kuhakikisha baadhi yao wanapatiwa huduma.
Licha ya matatizo yao, jamii na serikali kwa jumla haijayapa makundi  hayo uzito unaostahili katika suala la utoaji wa huduma za mahitaji muhimu na ya msingi, yakiwamo ya chakula, malazi, elimu na afya.
Katika picha na Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nusuru Yatima kilichoko katika manispaa ya Bukoba .
 Mlezi anawashukuru Wageni wote waliofika katika kituo hicho.
Mlezi wa kituo hiki anayesema;ukiwekwa utaratibu wa kuwapatia matibabu bure utawapunguzia hatari ya kupoteza maisha kwa maradhi yanayotibika.
Anasema kuna watoto wanaopoteza maisha kwa kutopatiwa matibabu kutokana na hali yao ngumu ya maisha, lakini anaamini kuwa serikali inaweza kuwaepusha na vifo iwapo itadhamiria
Mdau Ibra Cadabra kwa namna alivyo guswa na hali ya Watoto hao
Mrs Fide Pichani katika picha na Mmoja wa Watoto yatima
Misa fupi ya shukrani ikiongozwa na  Gioldina William , Binti anaye lelewa katika kituo hicho kwa sasa ni mwanafunzi wa Kidato cha tatu shule ya Sekondari Bilele
 Ndugu Musa na Ibra Cadabla wakiitia DUA inayo ongozwa na Mmoja wa Watoto hao
Dua ya Shukrani kwa Ugeni wao ikiendelea
Taswira watoto wakifurahia zawadi
 Kutoka 88.5 Kasibante Fm Radio DJ Slay pichani akishow love na Watoto yatima.
 Marafiki wa Karibu walio ongozana na Birthday Boy Fidel wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Watoto hao
Ustaadhi akitoa Dua ya Mwisho kabla ya Wageni kuondoka
Changamoto kubwa kituoni hapa ni Ukosefu wa huduma muhimu
Tatizo la kutowahudumia ipasavyo limesababisha watoto hao kukumbwa na changamoto nyingi, matokeo yake baadhi ya wanakimbia makazi yao na wengine kuwa watoto wa mitaani.
  Hivi ndivyo Mdau Fidel Blonzo Da One alivyo ungana na Mkewe na marafiki zake katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake na Watoto  yatima 
BUKOBAWADAU BLOG Tunatoa  Wito kwa watu wenye uwezo wa kifedha kujenga tabia ya kuwasaidia watu wenye uhitaji ili kuwapunguzia ukali wa maisha.
 Baada ya tukio hili Mdau Fidel ameendelea na hafla ya Chakula cha usiku nyumbani na kuwaalika sehemu ya marafiki zake .
 God bless you Mr. Fidel and your family and the rest of your life!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau