Bukobawadau

NI CHANGAMOTO BUKOBA YETU OCT 6,2014 !

.
 Taswira mbalimbali Mjini Bukoba, Mji  ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Kagera.
 
Bukoba ni Mji mzuri kwa vitu vya asili  (naturally) ndio uzuri wake. Anzia hali ya hewa, vyakula vya asili, maji/mto kila baada ya kilomita zisizozidi mbili,ni vitu vinavyopelekea Mji wetu kupendeza na kuvutia.
Ingawa kuna dhana potofu kuwa maendeleo yanapimwa kwa uzuri wa majengo na miundombinu nyingine iliyoko mijini.Mfano,kama jiji la Dar ni zuri basi hata wenyeji wenye asili kama wazaramo watakuwa wameendelea...,Ukweli ni kwamba Kigezo hicho siyo kamilifu na hakionyeshi hali halisi.
  Ndivyo inavyo onekana katika Mji wa Bukoba,Mji uliopo nyuma kimiundombinu lakini
miundombinu ya vijijini na mwananchi mmoja mmoja uko mbele sana
 Akiongea na Bukobawadau Mr.Ben Mulokozi aliyepo mjini hapa kwa ajili ya kukagua miradi yake amesema;'Wakati umefika sasa wana-kagera kuhakikisha tunaitafuta ELIMU popote pale ata Ulaya ikibidi.'
 Mr.Ben Mulokozi anaendelea kutoa angalizo kwa Wahaya  wenzake ni kuendeleza harakati za kutafuta  Pesa na kuimiliki ili kuepuka kuwa watumwa wa Wengine!!
Mr. Jamal Kalumuna anafika kusalimiana na Mr Ben Mulokozi
Katika meza ya pamoja usiku wa Jana Oct 6,2014.
Rais wa COSAD Tanzania Ndg Smart Baitani akifurahia siku na rafiki wake wa karibu Ndugu Pajero
Wadau katika picha ya pamoja
Mzee Bayona, Mdau Rama RMK na Mr Ben Mulokozi ambapo yeye  kama Real Estate  'property deals' aka (Binuzi)ameendelea kuwahasa wanakagera wajaribu kuwekeza Nyumbani
Hii leo inaonyesha Sehemu ya  Wahaya wenye uwezo hawakai hapo mjini kama unavyoweza kudhani bali wanaishi au wamejenga Vijijini
 Prince IP Motel eneo la biashara lenye umaarufu mkubwa Mjini Bukoba
Mkoa wa Kagera ulisifika kuwa na wasomi wazuri,wananchi wenye kipato ila sasa umekuwa mkoa masikini kupita kiasi,elimu iliyodorora, hakuna tena Nshomile hii tunaitowa kama changamoto,uchumi umedororo,mabati na cement  bei mara mbili
Pichani ni viwanja vya Golf vilivyojengwa  wilayani  Missenyi nyumbani kwa Malinzi ikiwa ni sehemu ya kitega uchumi.Tayari club house imejengwa,baadae itajengwa hotel ndogo, nia ikiwa ni kupafanya pawe kivutio cha utalii kwa eneo letu hili la kaskazini magharibi mwa ziwa victoria.
Eneo hili tayari wageni wanapaulizia na wengi wanakuja kucheza wakitokea nchi mbali mbali.
 Nchi nyingi duniani zinatumia golf course kama kivutio cha utalii,'hayo aliyadhibitishal Ndg Malinzi
 Taswira maeneo mbalimbali ndani ya Mji wa Bukoba.


Next Post Previous Post
Bukobawadau