SIKU YA MWALIMU DUNIANI KITAIFA MKOANI KAGERA LEO 5/10/2014 ;Walimu Kuundiwa Tume ya Utumishi Wao na Bodi ya Fani ya Ualimu ifikapo 2015
WAZIRI MKUU PINDA ASEMA
SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA WATUMISHI WALIOHAKIKI MADENI HEWA YA WALIMU NA
KUISABABISHIA SERIKALI HASARA
·
Walimu
Kuundiwa Tume ya Utumishi Wao na Bodi ya Fani ya Ualimu ifikapo 2015
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amesema serikali
itawashughulikia watumishi wasiokuwa waadilifu waliohakiki madeni ya walimu
nchini na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 10 kwa kuwasilisha
madeni yasiyokuwa ya kweli kwa manufaa yao binafsi.
Waziri
Mkuu Pinda aliyasema hayo wakati akihutubia taifa kwa ujumla kwenye maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani iliyoadhimishwa
kitaifa mkoani Kagera Jumapili Octoba 5, 2014 katika uwanja wa Kaitaba Manispaa
ya Bukoba.
Waziri
Mkuu alisema kuwa serikali itachukua hatua kali kwa watendaji walioisababishia
hasara serikali kwa kutaka kujinufaisha wao wenyewe binafsi kupitia madai ya
walimu nchini wakati akijibu risara ya
walimu iliyosomwa mbele yake na Mwalimu
Yahya Msulwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
Katika
risara ya walimu waliiomba serikali kuyafanyia kazi kwa uharaka mambo makuu
muhimu kumi na moja, ikiwa moja ni Upandishwaji wa Madaraja kwa walimu kwa
wakati, Pili ni Mishahara midogo kwa walimu huku wakifanya kazi zaidi na
mishara maalumu kwa wakuu wa taasisi kama wakuu wa shule na waratibu na Maafisa
Elimu.
Tatu,
madeni ya walimu kulipwa kwa wakati, nne ni uhaba wa nyumba za walimu, tano ni
mchakato wa utoaji elimu bora nchini,
vyou kudaili wanafunzi wa fani ya ualimu wenye vigezo kama fani nyinginezo,
sita ni kuhusu janga la UKIMWI kwa
walimu, Saba ni kuhusu serikali kuunda chombo kimoja cha ajira na Huduma kwa
walimu.
Nane,
ni mabadiliko ya mafao ya Pensheni kwa walimu kwa kutumia kanuni mpya ya SSRA,
jambo la tisa ni kuhusu kuboresha idara ya ukaguzi wa shule, kumi ni mpango wa
Matokeo Makubwa sasa kuihusisha elimu kwa raslimali fedha na raslimali watu. Mwisho
ni kuhusu ukosefu wa umakini kwa baadhi ya watendaji wa wanaohudumia walimu
katika ngazi za Wizara na Halamashauri
Waziri
Mkuu Pinda akijibu hoja hizo alisema serikali inaendelea kuzitatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili walimu nchini lakini akasema matatizo hayo yanatokana
na kuongezeka kwa huduma za elimu nchini pia ikiendana na ongezeko la walimu
wanaoongezeka kulingana na mahitaji katika sekta ya elimu.
Mhe. Pinda alisema mwaka 1961 wananfunzi wa shule
za msingi walikuwa 486,470 na waliongezeka hadi 8,419,305 mwaka 2010 sawa na
ongezeko la wastani wa wanafunzi 149, 676.1 kwa mwaka. Shule za Msingi
zimeongezeka kutoka 3,000mwaka 1961 hadi 15,816 mwaka 2010 sawa na ongezeko la
shule 241.8 kila mwaka.
Aidha
idadi ya walimu imeongezeka kutoka 9,885 mwaka 1961 hadi 165,856 mwaka 2010
sawa na wastani wa ongezeko la walimu
2,942.8 kwa mwaka. Pia madarasa
yameongezeka kutoka 3,100 mwaka 1961hadi
110,342 mwaka 2010 sawa na wastani wa ongezeko la madarasa 2,023.4 kila mwaka .
Waziri
Mkuu pia alisema matatizo mengi ya walimu yanasababishwa na kutotumia TEHAMA
(Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ) katika kushughulikia masuala mbalimbali
yanayowahusu walimu na ndiyo maana kero nyingi zinajitokeza mara kwa mara
lakini serikali imejipanga kulishughulikia tatizo hilo.
Vilevile
Waziri Pinda akijibu risara ya walimu nchini alisema kuwa serikali tayari
imekubaliana na ukweli kuwa utumishi wa walimu ni zaidi ya asilimia 50 ya
watumishi wote nchini kwa hiyo tayari serkali imekubali kuunda Tume ya Utumishi
wa wa limu (Teachers Service Commission) ili kushughulikia masuala ya walimu.
Aidha
serikali itaunda chombo kama Bodi ya
walimu ili kuifanya fani ya ualimu kutambulika kama fani zingine nchini
alisistiza Waziri Mkuu, ikiwa ni pamoja kuiunda upya TSD na kuiwezesha idara ya
ukaguzi wa shule kukidhi viwango katika kuimarisha elimu nchini.
Serikali
pia inaangalia uwezekano wa kuingia ubia na mashirika binafsi kuona kama
itatatua tatizo la nyumba za walimu ili walimu wapate makazi bora. Pia serikali
imeunda shirika jipa Watumishi Housing ili kuhakikisha watumishi wa umma
wanapata makazi bora kwa kujenga nyumba zao wenyewe kwa mikopo nafuu kutoka
Watumishi Haousing. Alisistiza kuhusu juhudi za serikali Mhe. Pinda.
Akihitimisha
hotuba yake Waziri Mkuu Pinda alisema kuhusu ukosefu wa umakini kwa baadhi ya
watendaji wanaohudumia walimu katika ngazi za Wizara na Halamashauri limekuwa
ni tatizo kubwa nchini kwani watendaji wengine wanankuwa na roho mbaya bila
sababu na kukataa kusikiliza shida za walimu lakini serikali inapobaini
hushughulikia suala hilo mara moja.
Siku
ya Mwalimu Duniani huadhimishwa tarehe 05 Oktoba kila mwaka. Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu yalianzishwa
rasmi na Shirikisho la Walimu Duniani (EI) mwaka 1993. Kwa Tanzania maadhimisho
ya Siku ya Mwalimu ni mara ya tatu kuadhimishwa mwaka 2006 yalifanyika Mkoani
Mtwara, mwaka 2010 yalifanyika mkoani Ruvuma na Mwaka huu 2014 mkoani Kagera.
Maadhimisho
ya Siku ya Mwalimu Duniani hufanyika kila baada ya miaka mitatu aidha kaulimbiu
ya Mwaka huu ilikuwa nia “Invest in the future/Invest in Teachers maana
yake kwa tafsiri ni Wekeza kwa maisha ya baadae/Wekeza kwa Mwalimu.