Bukobawadau

SKYLIGHT BAND YAENDELEA KUBAMBA NA MUZIKI WA LAIVU JIJINI DAR.

DSC_0167
Kikosi kazi cha Skylight Band kikiongozwa na mkongwe wa muziki wa Live Joniko Flower, Meneja wa Band Aneth Kushaba AK47, Sam Mapenzi na Sony Masamba kwa pamoja wakiwapa raha mashabiki wa bendi hiyo (hawapo pichani) kwenye kiota cha maraha cha Thai Village Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita ambapo leo wataendelea kutoa kuwaburudisha mashabiki wake kama kawaida kuanzia saa tatu usiku.
DSC_0088
Wanaume wa shoka wa Skylight Band kutoka kushoto ni Joniko Flower, Sony Masamba na Digna Mbepera wakionyesha mbwembwe zao za kulisakata sebene kwa mashabiki wao, ambapo jioni ya leo watakuwepo kama kawaida kwenye kiota cha maraha Thai Village.
DSC_0102
Skylight Band wakiserebuka na burudani yao kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita.
DSC_0113
Unajua siri ni nani anayemfanya Aneth Kushaba AK 47 kung'ara katika mambo ya Make Up?? si mwingine mfollow Instagram @timelesstz ukapendeze kama AK47.
DSC_0319
Pale Mashabiki wanapokunwa na burudani ya Skylight Band.
DSC_0118
Vocal zikiendelea kuporomoshwa kwa mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0027
NABOLINGOOOOO....! Binti mwenye kipaji cha pekee na sauti ya kumtoa nyoka pangoni Digna Mbepera akitoa burudani kwa mashabiki wanaojumuika na Skylight Band kula bata kila siku za Ijumaa ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0178
Sam Mapenzi akifanya yake jukwaani kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata kitu roho inapenda.
DSC_0214
Mmoja wa mashabiki wakubwa wa Skylight Band akishow love mbele ya camera yetu huku wengine wakijinafasi kwa raha zao pale kati.
DSC_0256
Hashimi Donode aliamua kushaka jukwaani na kujumuika na baadhi ya wapenzi wa Skylight Band kwenye dancing floor.
DSC_0270
Raha zote hizi zinapatikana kila Ijumaa ndani ya Thai Village USIKOSE: Joniko Flower akiwaduarisha mashabiki wa Skylight Band walifurika kuianza week end yao na bendi ya kijanja ambayo ni habari ya mujini kwa sasa.
DSC_0265
Mashabiki wa Skylight Band wakijinafasi na mduara shurti wa nyuma aende mbele na wa mbele aende nyuma.....!
DSC_0263
Umati wa mashabiki wa Skylight Band ukiburudika na hii yote ni kutokana na burudani yenye viwango kutoka kwa waimbaji na wapigaji wa bendi hiyo.
DSC_0285
Wakinadada wakizungusha hizo nyonga zao. #MaunoYaKumwagaRadhi.
DSC_0289
TOPHY Bass akilicharaza gitaa huku Daudi Tumba akizichapa Tumba zake kwa ustadi kabisa.
DSC_0352
Calvin Michael a.k.a DJ-K'FLIP wa Jembe Beach Resort na Club Jembe anahusika kwenye moja na mbili kuendelea kuwapa bata mashabiki wa Skylight Band baada kumalizika kwa muziki wa Live ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0355
DJ-K'FLIP wa Jembe Beach Resort na Club Jembe ya jijini Mwanza akishow love na Joshua Ndege.
DSC_0361
Kutoka kushoto ni Rais wa Wanamanyoya Family a.k.a #Sultan Gijegije, Eddievied na Luhano Lupogo wakiwakilisha #Wanamanyoya na ukodak.
DSC_0299
Mdau Andrew akishow love na warembooozzzz walipokuja kula bata na Skylight Band.
DSC_0347
Aneth Kushaba AK47 akishow love na Kaka yake Man Kushaba aliyekuja kushuhudia kipaji cha dada yake.
DSC_0298
Birthday Boy Professor Kingu (kushoto) akipata ukodak na mdau wa Skylight Band David.
DSC_0346
Birthday boy mwingine mratibu wa Skylight Band Lubea (kulia) akipata ukodak na Babu wa Kitaa na mdau.
DSC_0136
Man kushaba (kushoto) akishow love na marafiki.
DSC_0150
Mdau Faraja Fares (kushoto) akipata ukodak na marafiki.
DSC_0186
Divas wa Skylight Band wakipata ukodak.
DSC_0120
Wanamanyoya Family wakiwa na Rais wao Sultan Gijegije wa Oman.
DSC_0328
Mdau kubwa wa Skylight Band Jimmy JO akipata ukodak na Hashim Donode wa Skylight Band.
DSC_0333
DSC_0357
Sam Mapenzi wa Skylight Band akishow love na mashabiki wake.
DSC_0175
Blogger King Kif akishow love na wadau wa Skylight Band Ijumaa iliyopita.
DSC_0330
Hashim Donode na wadau wakubwa wa Skylight Band.
DSC_0148
Wadau wa Skylight Band wakipunga upepo kwenye bustani ndani ya kiota cha Thai Village.
Next Post Previous Post
Bukobawadau