Bukobawadau

GHAFLA UONGOZI KCU (1990) LTD WAPIGWA CHINI!!

Mkutano wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kagera KCU 1990 LTD uliofanyika leo Ijumaa Nov 21,2014 katika ukumbi wa Bukoba Coop zamani Yaasira kwa Siri na kuibuka na mabadiriko makubwa ambapo serikali kupitia kwa Mrajisi wa mkoa imetoa taarifa kuwa mwenyekiti John Binunshu na wajumbe wa bodi nzima ya KCU hawapaswi kuogombea nafasi za uongozi ndani ya Chama hicho.
Zoezi lililofuata Wajumbe wakaingia katika mchakato wa kuundwa kwa bodi mpya na kumchagua Ndgu Frank Muganyizi Theophil kuwa mwenyekiti na Ndg Ignas Bantanuzi kachaguliwa kama makamu Mwenyekiti.
 Katika mchakato huo,Wajumbe ni pamoja na Ndg Sadru Nyangasha pichani kushoto,Festo Paulo ,Sylvanus Muhyoza ,Projestus Ban  na Winfrida Kyombo.
CREDIT:harakatinews
Next Post Previous Post
Bukobawadau