MAPOKEZI YA MKUU WA MKOA MPYA NOV 14,2014
Mkuu
mpya wa Mkoa wa Kagera Bwana John
Mongella aliyeteuliwa na Rais Jakaya
Kikwete Novemba 5, 2014 kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera amewasili rasmi mkoani hapa
na kupokelewa na kukabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake Kanali Mstaafu
Fabian Inyasi Massawe.
Katika hafla fupi leo tarehe 14/11/2014 Kanali Mstaafu Fabiani Massawe alimsomea taarifa ya maendeleo ya mkoa Mhe. John Mongella na kumkabidhi taarifa hiyo pamoja na taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya serikali katika mkoa wa Kagera mwaka wa fedha 2014/15, na taarifa ya malengo ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2014/15
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Bi Costancia Buhiye, Mh. Massawe kulia ni Mkuu wa Mkoa mpya Mh. John Mongella
Kwa pamoja wakitembea Kuelekea Mapokezi Uwanja wa Ndege wa Bukoba
Mheshimiwa John Mongella Akivishwa Skafu
Katika utambulisho na Viongozi mbalimbali waliofika kumpokea.
Mh.Mkuu wa Mkoa akisalimiana na Sheikh wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta
Mkuu wa Mkoa mpya Mh. John Mongella akisalimiana na Afisa Uvuvi Ndg Apolinary Kyojo
Afisa mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Kagera Kapten Alex Katama akimkumbatia kwa furaha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mongella
Sehemu ya Wadau waliofika kumpokea Mkuu wa Mkoa Mpya Mh.John Mongella
Mkuu wa Mkoa Mh. John Mongella akitambua uwepo wa mwakilishi wa wanahabari Ndg Prudence Kibuka.
Burudani ya Ngoma maalum kwa ajili ya Mapokezi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mongella
Mheshimiwa John Mongella akisaini Kitabu cha Wageni Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
NDIYO WALIYOJIRI WAKATI MKUU MPYA WA MKOA WA KAGERA AKABIDHIWA RASMI OFISI NA MTANGULIZI WAKE KANALI MSTAAFU FABIAN MASSAWE NOV 14,2014
Katika hafla fupi leo tarehe 14/11/2014 Kanali Mstaafu Fabiani Massawe alimsomea taarifa ya maendeleo ya mkoa Mhe. John Mongella na kumkabidhi taarifa hiyo pamoja na taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya serikali katika mkoa wa Kagera mwaka wa fedha 2014/15, na taarifa ya malengo ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2014/15
Kanali
Massawe pamoja na kusoma na kukabidhi taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Kagera
hakusita kuzitaja changamoto zinazoukabili mkoa kwa sasa ambazo ni Wahamiaji
haramu hasa katika wilaya za Ngara, Kyerwa, Karagwe na Missenyi. Magendo ya
mazao na hasa kahawa, nafaka, mazao ya misitu, bidhaa mbalimbali hufanyika
kwenda nchi jirani.
Kilimo chetu kinakabiliwa na uzalishaji mdogo (tija);
matumizi duni ya pembejeo na zana za kilimo; uhaba wa maafisa ugani na magonjwa
hatari ya mimeaUfugaji nao bado ni wa kiasili wa ng’ombe aina ya ankole ambao
uzalishaji wake wa nyama na maziwa ni duni;
Upungufu wa miundombinu ya mifugo
kama majosho; magonjwa ya mifugo. Wavuvi wengi kutumia zana za asili kuvulia
samaki. Michango ya
halmashauri katika bajeti zake ni kati ya
2% hadi 4% ya bajeti nzima ya Halmashauri hizo. Kwa hiyo hali ya utegemezi ni kubwa sana na
hii inazipunguzia uwezo wa kuchangia katika maendeleo na utoaji wa huduma za
kuridhisha.
Mheshimiwa John Mongella Akipokelewa na Katibu Tawala Mkoa Bw. Nassor Mnambila na Kanali Mstaafu Massawe
Akikiri
kupokea ofisi na kuanza kuchapa kazi kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Kagera
Mkuu wa mkoa Mheshimiwa John Mongella
alihaidi kuendeleza jitihada alizokuwa akizifanya Kanali Massawe katika
kuwaletea wananchi maendeleo kwa
kushirikiana na watendaji walioko chini yake na wadau mbalimbali wa mkoa.
Pili,
Mhe. Mongella alitoa angalizo kwa watendaji wa serikali kuhakikisha
wanawahudumia wananchi katika ofisi zao bila kutumia milolongo mirefu ya sheria
na taratibu. “Mwananchi hajui mambo ya standing order anachojali ni kupata
huduma kwa wakati bila kucheleshwa, kwahiyo punguzeni milolongo mirefu ya
utendaji wa kazi katika kutoa huduma.” Alisistiza Mhe. Mongella.
Tatu,
Mkuu wa Mkoa Mongella alisistiza kuwa hapendi kufanya kazi kwa maneno mengi
bali kwa vitendo na kuona , “Kama ni vyumba vya maabara nataka kuonyeshwa
vyumba au kama ni zahanati nataka kuonyeshwa zahanati na siyo maneno maneno
tu.” Aliongeza Mkuu wa Mkoa Mongella.
Mwisho
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella alikemea na kutoa angalizo kuacha kutumia
siasa au kuendekeza siasa katika maendeleo ya wananchi, alisema waache
wanansiasa wafanye siasa zao lakini si katika kuwaletea wananchi maendeleo
ambalo ndilo jukumu kuu la viongozi na watendaji wa serikali.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa
wa Kagera na Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha na
anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa tangu
uhuru mwaka 1961.
Mkuu Mpya wa Mkoa Bwana John Mongella akipokea Nyaraka na Kukabidhiwa Ofisi Rasmi na Mtangulizi wa Kanali Mstaafu Fabian Massawe.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akikabidhi Nyaraka zenye taarifa ya Mkoa kwa Mkuu wa Mkoa mpya Mh. John Mpngella,anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bi Costancia Buhiye.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Bi Costancia Buhiye, Mh. Massawe kulia ni Mkuu wa Mkoa mpya Mh. John Mongella