MGOGORO WA KISIASA BUKOBA MAHAKAMA YATOA HUKUMU MPYA NOV 11,2014
Mahakama ya wilaya ya bukoba Mapema ya Jumanne Nov 11,2014 imetoa
hukumu mpya kuhusiana na mgogoro wa manispaa ya bukoba unaoendelea
kulindima katika manispaa hiyo.
Katika maamuzi yake hakimu wa
mahakama hiyo Ndugu Samweli Maweda ameagiza naibu meya wa manispaa ya bukoba
Ndg Alixandar Ngalinda kuendesha vikao vyote vya halmashuri hiyo na
vikao kuendelea kama kawaida.
Awali Meya wa Bukoba Anatory Amani aliweka pingamizi katika mahakama hiyo
kuzuia kufanyika kwa vikao vyovyote mpaka atambuliwe kuwa ndiye meya wa
Bukoba na ashiriki kuendesha vikao vya madiwani.
Pichani anaonekana Mh.Jeanifer Murungi Kichwabuta akiteta jambo wakili wa TAMISEMI anayemtetea Mkurugenzi wa manispaa ya BukobaMakamu Meya wa Manispaa Bukoba Mh. Ngalinda akiongea mbele ya mwanahabari
Hata hivyo hakimu amesema ‘Wananchi wanashindwa kupata maendeleo kwa sababu vikao havifanyiki kisa ni kesi ,hivyo mahakama inaamua kwamba kuanzia sasa vikao vifanyike chini ya naibu meya na suala la kesi ya Msingi juu ya kama Anatory Amani ni Meya au la litaamuliwa baadaye katika kesi ya msingi itakayoanza kusikilizwa januari 19,2015.
Hata hivyo taarifa zilizotolewa na mawakili wa serikali na Aron Kabunga anayemtetea Dk Aman kwa nyakati tofauti wamedai kuwa wanaridhika na uamuzi huo.
Wameongeza kuwa katika vikao hivyo madiwani tisa waliosimamishwa wataendelea na adhabu yao hadi uamuzi toafuti na huo utakaotaolewa na mahakama au vyombo vingine na kuwa hawataruhusiwa kuudhuria vikao hivyo na katika vikao masuala ya mgogoro huo hayatajadiliwa bali watahusika kujadili masuala ya maendeleo tu.
VIA HARAKATINEWS.