MTAZAMO WA KISAIKOLOJIA KUHUSU MA HOUSE GIRL KUWANYANYASA WATOTO WETU
(HII NI KUFUATIA VIDEO YA HOUSE GIRL AKIMTESA MTOTO MDOGO INAYOTEMBEA KWENYE MITANDAO)
Inabidi pia wazazi kufahamu kuwa wafanyakazi tunaowaajiri wanatoka katika backgrounds tofauti tofauti sana, na kwa jinsi wengine walivyokuzwa, kunyanyasika au kuonewa au kunyimwa haki labda hadi ndoto zao kukatishwa wakajikuta wanakuwa wafanyakazi wandani tofauti na walivyotamani, ndivyo mianya ya hasira, visasi na machungu hupanuka na kuishia kwa watoto wetu wapenzi tuliowaacha wakae nao nyumbani. Huku ukidhani kuwa mwanao yuko salama kumbe yuko kwenye mikono ya muhanga wa maisha ambaye anaishi chini ya dari yako ili tu ale na alale na apate hela kidogo lakini moyoni mwake yamkini mazingira yameshamuandaa kuwa jitu na sio mtu.
Ni vema tukafahamu historia za wadada na wakaka tunaowaajiri na tukaishi nao chini ya dari moja, unaweza kumuliza katika kupiga story za kawaida tu, jifunze kuwafanya wawe marafiki ili waweze kuelezea matukio yaliyowahi kuwasibu maishani mwao. Usimuangalie tu kama mfanyakazi kwasababu unamlipa bali muangalie kama mtu anayekaa na watoto wako, tena anayekaa muda mrefu kuliko wewe. Watu hawa wananafasi kubwa sana ya kuwaathiri watoto wetu katika maisha mazima, tena athari hizi zinaweza kuendelea hadi utu uzima wao. Achana na kupigwa au kuteswa kwa watoto wetu, hivyo angalau unaweza kuviona kwa macho, vipo vitu tele tena very sensitive ambavyo huwezi kuviona wala kuvisikia lakini vina athari kubwa sana kwa watoto wetu kutoka kwa wafanyakazi hawa. Zaidi ya yote tumruhusu Mungu kuwa mlinzi mkuu kwa watoto wetu kwasababu wenyewe hatuwezi hii kazi.Tuwe macho wapendwa - Dr. Chris Mauki