MTERA SHOOTING MABINGWA LUKUVI CUP 2014 KATA YA MIGOLI YAIGAGADUA HOME BOYS MBELE YA WAZIRI NKAMIA
Wachezaji wa timu ya Mtera wakiendelea kuumiliki mpira katikafainali ya Lukuvi Cup kata ya Migoli Mtera |
Mabingwa wa Lukuvi Cup timu ya Mtera wakimiliki mpita |
Mchezaji wa timu ya Home Boys akiwa chini baada ya mchezaji wa timu ya Mtera kuupiga kichwa mpira uliokuwa ukigombewa |
Mashabiki wakifuatilia mchezo huo |
Naibu waziri Nkamia akiwa na makombe ya Lukuvi Cup |
Uwanja ukiwa umezungukwa na mashabiki kabla ya mchezo kuanza |
Shangwe ya ushindi |
waziri Nkamia akimkabidhi zawadi mchezaji wa timu ya MTERA |
waziri Nkamia akiwa na mchezaji bora wa timu ya mtera Bw.mzambia |
Waziri Nkamia akimkabidhi kombe kepteni wa Home Boys
Mashabiki wakifuatulia zoezi la zawadi |
Na MatukiodaimaBlog
MTERA Shooting yaibuka mabingwa Lukuvi Cup 2014 kwa kata ya Migoli jimbo la Isimani baada ya kuifunga timu pinzani ya Home Boys kwa jumla ya magoli 4-1 katika mchezo wa fainali ulioshuhudiwa na mgeni rasmi naibu waziri wa habari ,vijana ,utamaduni na michezo Juma Nkamia.
MTERA Shooting yaibuka mabingwa Lukuvi Cup 2014 kwa kata ya Migoli jimbo la Isimani baada ya kuifunga timu pinzani ya Home Boys kwa jumla ya magoli 4-1 katika mchezo wa fainali ulioshuhudiwa na mgeni rasmi naibu waziri wa habari ,vijana ,utamaduni na michezo Juma Nkamia.
Mchezo
huo uliochezwa juzi katika uwanja wa Migoli Mtera uliokuwa na
upinzani wa hali ya juu kwa timu zote kutokana na kushindwa
kuonyeshana ubabe dakika 90 za mchezo kwa timu hizo kutoka sare ya
goli 1-1 kabla ya kumsaka mshindi kwa mikwaju ya penati ambayo
iliiwezesha timu ya Mtera Shooting kuigagadua (kuifunga) Home Boys
kwa jumla ya magoli hayo 4-1 ambayo yaliiwezesha kutwaa kombe na
kiteta cha pesa taslim kiasi cha Tsh milioni 1 kutoka kwa mbunge wa
jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa nchi ofisi ya
waziri mkuu sera na uratibu wa bunge.
Kbala
ya dakika 90 za mchezo kumalizika timu ya Mtera Shooting iliweza
kuwanyanyua mashabiki wake baada ya kujipatia goli la kwanza dakika ya
86 kwa mkwaju wa penati goli lililowekwa nyavuni na Mtei Mlimbwa
huku dakika ya 88 Frank Jackson
aliweza kuisawazishia timu yake ya Home boys goli hilo hivyo timu
hizo kutoka uwanjani dakika 90 kwa bila mbabe kujulikana.
Hali
hiyo iliweza kupelekea mashabiki wa kila timu na wachezaji kupigwa
na butwaa ya nani kutwaa kombe hilo kabla ya mwamuzi kutumia njia ya
matuta kumpata mshindi ambae alitokana na ujuzi wa kugusa nyavu
za mwenzake.
Akikabidhi
zawadi kwa mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu, Naibu Waziri wa
habari, vijana, utamaduni na michezo, Juma Nkamia,ambaye ndiye alikuwa
mgeni rasmi, alisema kuwa vijana wengi Tanzania wanapenda michezo japo
bado kuna tatizo kubwa kwa viongozi wa michezo hususani walimu wa timu
kwa kutokuwa na mafunzo ya ualimu wa timu.
Mapema
katibu wa mbunge Lukuvi ,Thom Malenga alisema kuwa lengo la mbunge
Lukuvi kuanzisha mashindano hayo ni kuweza kuhamasisha michezo katika
jimbo hilo na kuwafanya vijana kuepukana na matumizi ya madawa ya
kulevya pamoja na mambo mengine ambayo yanaweza kuwasababishia kupata
maambukizi ya VVU.
Mbali
na hilo alisem akuwa kupitia michezo wananchi wanakuwa pamoja na
kuondokana na masuala ya itikadi vya vyama wakati wa kufanya
shughuli za kimaendeleo.
Pia
alisema mbali ya mashindano hayo ya ngazi ya kata pia ameanzisha
mashindano ya ngazi ya tarafa ambapo bingwa atazawadiwa Power tilla
kwa ajili ya kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali katika tarafa.
Waziri
Nkamia
akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi wa mashindano hayo
alisema kuwa uamuzi uliofanywa na mbunge Lukuvi katika kuanzisha
michezo ni uamuzi wa kupongezwa kwani mbali ya kutekeleza ilani ya CCM
katika michezo bado amewawezesha vijana kupata fursa ya kuonyesha
vipaji vyao ili kupata nafasi ya kuchezea timu kubwa zaidi .
Hivyo
alisema katika mchezo huo kwa upande wake amependezwa na kiwango cha
mchezo cha mchezaji wa timu ya Mtera pia alisema kuwa mbunge Lukuvi
ametenga zaidi ya Tsh milioni 30 kwa ajili ya mashindano ya soka katika
jimbo hilo la Isimani na yeye kama waziri mwenye dhamana ya michezo
amependezwa zaidi na jitihada hizo
" Mimi katika kuunga mkono jitihada hizi za Lukuvi nawaahidi kuwa nitawasiliana na Lukuvi ili mabingwa wakacheze na timu yangu jimboni Kondoa mkoani Dodoma na mchezo mwingine waje wacheze hapa Mtera hapo vipi ".
Katika
mashindano hayo NKamia alimkabidhi mshindi wa kwanza kombe na fedha
taslimu shilingi milioni 1 huku mshindi wa pili akuikabidhiwa kombe na
shilingi
500,000,mshindi wa tatu akipewa Tsh 250,000 na mchezaji bora kutoka
timu ya Mtera akipewa Tsh 100,000