Bukobawadau

NAIBU WAZIRI KAIKA TELELE AFUNGA RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA UVUVI DUNIANI YALIYOFANYIKA MANISPAA YA BUKOBA MKOANI KAGERA

Maadhimisho ya siku ya Uvuvi duniani yalioadhimishwa kitaifa mkoani Kagera kuanzia  Novemba 19, 2014 na kuambatana na maonyesho mbalimbali kutoka katika sekta ya uvuvi yalihitimishwa rasmi na Naibu waziri wa Maendeleo ya mifugo na Uvuvi Kaika Saning’o Telele  jana tarehe 21/11/2014.
 Akifunga maadhimisho hayo Naibu Waziri Telele alisema sekta ya uvuvi ni miongoni mwa sekta za uzalishaji ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi wa taifa la Tanzania ambapo sekta hiyo inawahusisha wananchi wengi na kutoa ajira, lishe bora, kipato na kuchangia katika pato la taifa.
Naibu Waziri Telele alisema kuwa katika mwaka 2012, jumla ya tani 365,023.40za mazao ya uvuvi yenye thamani ya shilingi trilioni 1.3 zilivunwa nchini ikilinganishwa na tani 375,160 za mazao ya uvuvi yenye thamani ya shilingi trilioni 1.4 zilizovunwa mwaka 2013.
Aidha pamoja na kupungua kwa samaki  nchini lakini nguvu ya uvuvi imeongezeka kutoka wavuvi 182,741 waliotumia vyombo vya uvuvi 56,985 mwaka 2012 hadi wavuvi 183,431 waliotumia vyombo vya uvuvi 57,385 mwaka 2013.
 Katika kilele hicho cha maadhimisho ya siku ya uvuvi duniani pia wavuvi walitoa changamoto wanazokabiriana nazo katika kuteleza majukumu yao kama kuvamiwa na maharamia ziwani wakivua, halamashauri za Wilaya kutotenga bujeti za kuwaendeleza wavuvi, Taasisi za kifedha kutotambua uwekezaji wa wavuvi ili kuwapatia mikopo ya kujiendeleza.
Akijibu utatuzi wa changamoto hizo Naibu Waziri Telele alisema wizara yake imeandaa na kuanza kutekeleza program ya kuendeleza sekta ya uvuvi kwa kipindi cha mwaka 2011/2012 hadi mwaka 2015/2016, Programu hiyo inajumuisha mambo makubwa manne  yafuatayo;
Usimamizi endelevu wa rasilimali za uvuvi, Matumizi endelevu ya rasilimali uvuvi na masoko, tatu Uendelezaji wa ukuzaji wa viumbe kwenye maji na , nne Utafiti wa huduma za mafunzo na huduma za ugani ili kuhakikisha sekta ya uvuvi inakua kwa kasi na kuleta manufaa kwa wananchi walio wengi.
 Aidha Naibu Waziri Telele aliushukuru mfuko wa hifadhi wa NSSF kwa kuingia katika sekta ya uvuvi na kuanza kuwaelimisha wavuvi na kuwapa maono na elewe kuhusu huduma zitolewazo na mfuko huo pia alitoa wito kwa mifuko na taasisi nyinginezo kujikita katika sekta hiyo ili kuinua uchumi wa wavuvi.
 Changamoto kubwa iliyojitokeza katika maadhimisho hayo ni kutoshiriki kwa kwa halmashauri  za wilaya za mkoa wa Kagera ambao Katibu Mkuu Waizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Yahana Budeba alisema  kuwa wizara italifanyia kazi suala hilo ili katika maadhimisho yajayo yaweze kuwashirikisha wadau wengi wa sekta ya uvuvi .
Kilele cha Maadhimisho hayo kiliambatana na michezo mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta ya uvuvi hasa wavuvi ambapo walionyeshana ujuzi wa kupiga makasia na kuogelea na washindi kupewa zawadi nono. Maadhimisho ya Siku ya Uvuvi Duniani hufanyika kila mwaka Novemba 21.
Next Post Previous Post
Bukobawadau