Bukobawadau

PITIA MAAZIMIO MAPYA WALIYOKUBALIANA WABUNGE KUHUSU SAKATA LA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW

Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe amesoma maazimio mapya ya Bunge kwa mujibu wa kamati maalumu iliyoundwa leo na kuhusisha CCM, PAC na UKAWA Azimio: Mamlaka ya uteuzi iwawajibishe na inashauriwa kutengua uteuzi wa Waziri wa Nyumba,
ardhi na makazi Prof Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo, Mwanasheria Mkuu wa serikali Jaji Werema, na Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati
na Madini Maswi
Azimio: Bunge liwawajibishe wabunge ambao ni sehemu ya bodi ya TANESCO na viongozi wa Kamati za Bunge Azimio: Mamlaka husika ziitangaze Benki ya Stanbic, Mkombozi na benki yoyote nyingine itakayogundulika kuwa zinahusika na utakatishaji wa fedha haramu Azimio: Kwa kuwa majaji walihusika, Rais aunde Tume ya kijaji ya uchunguzi na kuwasimamisha jaji Mujulusi na Prof Luhangisa Azimio : Serikali ipitie upya mikataba ya Umeme na itoe taarifa kabla ya kumalizika kwa mkutano ujao wa bunge la Bajeti Azimio : Serikali ichukue mitambo ya IPTL na iikabidhishe kwa TANESCO Azimio: TAKUKURU na Polisi wamchukulie hatua bwana Sethi, na kumfungulia mashitaka akithibitika Wasira: Tuamini kwamba haya yote ni kwa maslahi ya watanzania, CCM imeshirikiana na kambi ya
upinzani kufanya maamuzi sahihi.

Mbowe: Tumekaa kama Kamati kurudisha heshima na mshikamano wa nchi. Walioko serikalini wana wajibu wa kulinda rasilimali za nchi,Watekeleze wajibu wao kwa uadilifu.
Wassira: Nilikua miongoni mwa wajumbe sita kuwakilisha katika kikao cha maridhiano, jana hali ilikua mbaya sana na tulitoka katika mazingira yasiyoeleweka lakini kwenye binadamu hapaharibiki jambo kumbe tukitumia busara jambo gumu linakuwa rahisi. Tumebadilishana mawazo kwa uaminifu zaidi, kwa niaba ya CCM tunashukuru kwa mjadala na CCM imeshiriki katika kufikia maazimio. Jambo lolote lenye kuleta msukosuko katika nchi haliwezi kuwa sera ya CCM hivyo tunaomba wananchi wayaunge mkono hayo tuliyokubaliana. Kama Zitto alivyosema tumegusa kila muhimili lakini tumeyagusa kwa nia njema, naunga mkono hoja.
Next Post Previous Post
Bukobawadau