SALAAM ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MTENSA
Nimepokea
kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ndugu / rafiki
yetu Mutensa. Binafsi ninauchukulia ni msiba wa wana Kagera wote.
Marehemu Mutensa alikuwa ni mpambanaji aliyejitahidi kuibadilisha Bukoba
kwa jitihada za ujasitiamali. Ni miongoni mwa wazaliwa wa Bukoba ambao
kwao Bukoba ilikuwa ni kila kitu, kuwekeza Bukoba kuna changamoto
nyingi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake litukuzwe. Tumuombe Mungu
aipokee roho ya marehemu na ampatie pumziko la amani.
Anic Kashasha - Dar es Salaam
Anic Kashasha - Dar es Salaam