Bukobawadau

TASWIRA MSIBANI KWA MTENSA LEO ALHAMISI

Yaliyojiri mapema ya Leo katika msiba huu mkubwa uliotufika”. ... ambao kwa namna moja ama nyingine walio wengi nje na ndani ya Mkoa wa Kagera wameguswa na msiba huu”
 Kulia anaonekana Kaka Peter Mgisha ambapo kwa niaba ya  familia ya Marehemu Mtensa Leonard wanatoa  shukrani za dhati kwa jinsi ambavyo watu wengi wameguswa na msiba huu na kuonyesha upendo na ushirikiano wa hali ya juu katika kuwafariji, kutoa pole na hata kujitolea kwa hali na mali. Mwenyenzi Mungu aendelee kuwaongezea pale mlipotoa.
 Kaka Mkubwa E. Nyambo muda mchache baada ya kuwasili kushiriki katika shughuli ya kumuaga mpendwa wetu Marehemu Mtensa Leonard
anaonekana Mdogo wa Marehemu Mtensa, Ndugu Juvenary akifarijiana na Kaka E. Nyamba.
Hali ya simanzi  na majonzi vikiendelea kutawala
 Marehemu Mtensa Leonard enzi za uhai wake,aipokee roho yake na kuipa pumziko la amani..Cosad Tanzania Deeply Sad episode.Cosad Tanzania inapenda kusema hivi: "Kama Ujasilia Mali Ungekuwa Dini--(hasa ujasili wa kuwekeza sehemu zenye changamoto kari kama Bukoba)...This brave man, son of Bukoba would have been anointed a saint! We are saddened by those, as a result of his untimely demise can't put a bread on the table, those whose dreams are shuttered, those who had jobs through his entrepreneurial courage and now, they have to start a new page+RIP brave brother!.
 Kaka E. Nyambo na Super Mkude katika tafakuri juu msiba wa rafiki yao
 Mikakati na maandalizi ya Mazishi ya Marehemu Mtensa Leonard inaendelea vizuri, Bukobawadau Blog tunapenda kuwataarifu kuwa shughuli ya mazishi itafanyika siku ya Jumamosi Nov 22 majira ya saa 9 alasiri nyumbani kwa Marehemu Kyakailabwa ulipo msiba kwa hivi sasa
Tatu familia inategemea kufanya tukio la kumuaga Marehemu (last respect) siku ya Ijumaa ambapo mwili wa Marehemu utatolewa hospital mida ya saa 9 jioni kuelekea nyumbani kwake Kyakailabwa na katika hili tunawafahamisha wadau wa mji wajitokeza kuanzi pale government hospital

Bukobawadau Blog tutaendelea kuwafahamisha utaratibu mzima na mambo mengineyo! 
 Pichani kushoto ni Mdau Anic Kashasha, anasemaa;'Nimepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ndugu / rafiki yetu Mutensa. Binafsi ninauchukulia ni msiba wa wana Kagera wote. Marehemu Mutensa alikuwa ni mpambanaji aliyejitahidi kuibadilisha Bukoba kwa jitihada za ujasitiamali. Ni miongoni mwa wazaliwa wa Bukoba ambao kwao Bukoba ilikuwa ni kila kitu, kuwekeza Bukoba kuna changamoto nyingi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake litukuzwe. Tumuombe Mungu aipokee roho ya marehemu na ampatie pumziko la amani.'
Anic Kashasha - Dar es Salaam


Next Post Previous Post
Bukobawadau