Bukobawadau

AMSHA AMSHA KIJIJINI BUGANGUZI DEC 21,2014

Ni Jumapili tulivu Dec 21,2014, hali ya hewa ikiwa imetulia kijijini Buganguzi-Muleba tayari jua limezama , Kama kawaida yetu ni katika kukuangazia kinachojiri maeneo kadha wa kadha.
Tunafika Nyumbani kwa Mzee Tiba (pichani kushoto) hii ni sehemu ya kipengele maalum kijulikanacho kwa jina kama "Amsha amsha Desemba 2014"kupitia kupitia Bukobawadau Blog.
  Familia nzima ya Mzee Tiba kama kawaida kwa mwezi Desemba hukusanyika kwa pamoja Kijijini Buganguzi kwa ajili ya kusherekea Siku kuu pamoja na mambo mengineyo.
 Kama anavyo onekana na kitu 'headphone' akifurahia muziki
 Katika hali ya utulivu kwa ajili ya mipango mbalimbali
 Kwa ujumla maandalizi ya sikukuu yanaendelea vizuri kijijini hapa kama wanavyo onekana Wadau pichani wakiwa na nyuso za furaha ukizingatia na Ugeni uliopo!
Mwl. Lambart pichani Ndugu wa familia ya Mzee Tibaigana.
 Taswira nyumbani kwa Mzee Tiba.
 Maeneo mengine Jimboni kwa Mh. Charles Mwijage
 Amsha Amsha Kijijini Makongola, tunakutana na Ng'ombe wa ajabu na mkubwa kuliko  
 Hakika Ng'ombe huyu ni mkubwa.
 Kadadaa pichani akiwa kando kando ya barabara ya Bulyakashaju-Makongola katika kufurahia  Jumapili yake .
 Maeneo mengine mfumo bado huko hivi..'batter trade' (bihashara ya kubadirishana bidhaa).Pichani anaonekana Kijana akiwa na mzigo wa kuni kichani ,hana furaha kabisa !...lengo lake ni kuona kama atarejea nyumbani na chochote kama Ndizi,Unga au Sukari
Haaahh! Mambo ya Old School, tunavutiwa na kijana mwenye mpira wa kamba kichwani
 Eneo la Katanga,Camera inazoom Wasichana waliokuwa wakifua na wengine wakichota maji mtoni
Next Post Previous Post
Bukobawadau