BALOZI KAMALA AKAGUA HOTELI YA NYOTA TANO PATAKAPO FANYIKA KONGAMANO LA BIASHARA MWAKA 2015
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( wa pili
kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya
Afrika Rise ya Ubeligiji baada ya kukagua Hoteli ya Nyota tano ya
Chateau Du Lac patakapo fanyika Kongamano la Biashara na Uwekezaji
mwezi Aprili, 2015. Makampuni 500 kutoka Luxembourg, Ufaransa, Canada,
Switzerland, Dubai, Ubeligiji, Tanzania, Morocco, DRC na Algeria
yanatarajiwa kushiriki. Tanzania imekaribishwa kushiriki katika
Kongamano hilo na itapewa fursa ya kutangaza fursa za biashara na
uwekezaji zinazopatikana Tanzania. Kongamano hilo litafanyika jijini
Genval - Ubeligiji.