CHADEMA;SERIKALI ICHUKUWE HATUA WALIOHUSIKA NA WIZI AKAUNTI YA ASCROW
Chama cha demokrasia na maendeleo-Chadema- kimeitaka serikali
kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani viongozi waliohusika
katika wizi wa fedha katika akaunti ya Tegeta -Escrow- licha ya wengine
kuandika barua kujiuzulu wadhifa zao.
Akizungumza na waandishi wa habari, naibu katibu mkuu wa Chadema,
Mhe.John Mnyika amemtaka rais Jakaya Kikwete kuyafanyia kazi maadhimio
ya bunge ya kuwaondoa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria viongozi
hao, hata kama watajiuzulu nyazifa zao.
Akielezea uchaguzi wa serikali za mitaa, naibu katibu mkuu wa chama
hicho Zanzibar Bwana Salum Mwalimu amemtaka waziri wa tamisemi Mhe.
Hawa Ghasia kutangaza matokea chaguzi za serikali za mitaa kwa nchi
nzima badala ya kuwahachia viongozi wa vyama vya siasa kuendelea
kuwadanganya wananchi kuwa vyama vyao vimepata ushindi wa kishindo.
Kwa upande wake baadhi ya wananchi wameitaka serikali kufuatilia
ajira za wageni katika baadhi ya benki nchni kutokana na ongezeko la
wizi ambao yanaambatana na baadhi ya watendaji kujiuzulu nyadhifa zao
baada ya muda.