HAFLA YA KUMPONGEZA MWL-MARTHA BISHANGA YAFANA NDANI YA BUKOBA CO-OP..!!
Hafla ya kumpongeza Mwl. Martha Bishanga kwa kustaafu utumishi wa Umma yafana Sana,Hafla hii imefanyika Usiku wa jana Dec 12,katika Ukumbi wa Bukoba Co-Op Hotel.
Shughuli inaanza kwa furaha ..Wanafamilia wanaingia ukumbini
Namna hii wakicheza na kuimba wimbo wa 'Nani kama Mama'
Watoto wa Mstaafu mwalimu Martha Bishanga kama wanavyo onekana wakiingia kwa mbwembwe ukumbini na kupata mapokezi ya nguvu kutoka kwa waalikwa.
Kundi la Walimu linafuata likiongozwa na Mzee Manyama.
Sasa anaingia Ukumbini mstaafu Mwalimu Martha Bishanga akiwa amependeza ile mbayaa! Vazi refu alilovaa limemkaa vyema
Waalikwa ukumbini wakiwa wamesimama wakati Mstaafu akiingia Ukumbini
Mwalimu Martha Bishanga pichani kushoto na mpambe wake,ambaye ni rafiki yake karibu Mama Matungwa mtaalam wa Decoration::Advents Deco and Planning kama mtakavyo jionea kumbi umepambwa na kupambika ipasavyo
Mara baada ya mstaafu kuingia ukumbini, Shughuli ikafunguliwa kwa sala takatifu iliyo ongozwa na Bi Mecktrida Michael Pichani
EEEE BANA EEEE Muonekano wa Kitu Keki iliyotengenezwa na mtaalam wa fani Mama Simeo!!
Jamani pale kwenye kutoa sifa mtu na apewe sifa zake BUKOBAWADAU tunachoweza kusema hii ya leo ni kiboko Kwa Keki..Ni Sheeedah !!
Bi Georgia Kalikawe na Mama Lugusha pichani ni sehemu ya waalikwa
Meza mbalimbali za waalikwa walio hudhuria hafla hii ndani ya Ukumbi wa Bukoba Co-Op,
Kushoto ni Mh. Anathory Aman na Mkewe.
Kutoka katika familia za kichief ni Bi Anitha Rugalabamu na Mr Devo Rugaibura (Mr & Mrs Divo.
Kuvaa ni njia mojawapo ya kujiamini kwa mwanamke,Pichani anaonekana Bibie Laty katika 'Smile' Mtoto mkalee, mtoto msomi, ana pozi na muelewa!
Muonekano wa meza mbalimbali za waalikwa ukumbini.
Mwalimu Martha Bishanga akitoa Utambulisho.
Watoto wa Mstaafu Mwalimu Martha Bishanga pichani
Walimu wenzake katika Utambulisho
Pichani kulia anaonekana Mr. Mkayo
Kwa vazi hili Credit kwako Dada Hope Kazimbazi wa Makoko maarufu kama Manywele,tunakupa Credit kwa sababu kuna watu wanashindwa kutofautisha nguo ya kuvaa disco na kwenye party..!!
Katika hili na lile ndivyo mambo yanavyo endelea ukumbini hapo.
Mr & Mrs Anathor Amani wanapokea zawadi yao ya Keki
Zawadi kwa Kaka yake ambaye ndiye kiongozi wa Ukoo Dr. Bishanga.
Kwa niaba ya Mme wake Mzee Ngaiza Meneja wa KCU (1990)Zawadi inapokelewa na mwane mkubwa Ndugu Rweyemamu Victar Ngaiza
Mdau Samuel Stephen mwenyekiti wa Kamati ya Chakula mara baada ya kupokea zawadi ya keki kwa niaba ya kamati nzima ya maandalizi ya hafla hii.
Mwalimu Fabian naye anapokea zawadi ya keki
Shughuli ya kukabidhi zaidi ya Keki 20 kwa ndugu jamaa na marafiki likiendelea kwa kasi.
Bi Angel, Mrs Nyamoni baada ya kupokea zawadi ya keki ya Upendo kutoka mama Mzazi
Walimu wa Shule ya msingi Kashai,Shule aliyokuwa anafundisha Mwalimu Bishanga hadi kustaafu .
Mama Adventina matungwa akipokea zawadi yake ya Keki
Bi Editha katibu wa kamati ya maandalizi akikabidhiwa zawadi yake ya Keki
Watoto na wajukuu wa Mwalimu Martha Bishanga katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi yao ya Keki
Sehemu ya Watoto wa kuzaliwa na Mstaafu Mwalimu Martha Bishanga.
Mama Semeo na Mama Matungwa katika hili na lile wakati Mstaafu akiendelea kukabidhi zawadi ya keki kwa makundi mbalimbali kulingana na umuhimu katika maisha yake ya kazi mpaka kustaafu
Kuhusiana na Keki jamani mchakato ukiendelea
Juu ya Keki Hongera Sanamama Simeo,hongera Dada Angel na kamati yamaandalizi.
Anaonekana Bibie Editha wa Nicodemus kama kawaida ni mtu tabasamu wakati wote.
Kivutio kingine katika hafla hii ni Wanamama walivyo onyesha umahiri wa kufungua champagne.
Wakimpongeza mama yao mzazi
Bi Anjoy mara baada ya kumpongeza Mama yake Mzazi
Anaitwa Jamal Kalumuna
Bi Sharifa wa Athman ShaR wa Badru Mangi Saidi
Bi Jamila Jamal pichani kulia.
Pongezi zikiendelea kumiminika
Hakika watu wote wanaonekana wenye furaha katika kumpongeza mstaafu Mwalimu Bishanga.
Katika kuzoom anaonekana Mdau akifanya 'kutweet'
Mwanadada Sarah pichani
Katika hili na lile ndivyo anavyo onekana mmoja wa waalikwa Ukumbini
Kundi maarufu la Mwanadada Mery likiendelea kutoa burudani safi ya Ngoma za asili.
Star wa Usiku huu alikuwa Mr. Kilangani, aliyeweza kutoa historia ya Mstaafu Mwalimu Martha Bishanga kwa njia ya ushairi yaani sauti iliyo kati ya kuimba na kuongea tena kwa lugha ya asili "Kihaya'
Kibwakizo kikubwa katika ushairi huo kinasema ...'Martha Akanganyira Owomulikubona Omumaisho ganyu, Mwana wa ta Sebastiani Bishanga na ma Paulina Kokunywegeza, Omwabo ni Kiziba Kanyigo Omukyaro kwa Kikukwe...
'Orugandarwe Mulwanikazi nazira Ente ya Runya,naruga omumalembo nyarutembo... 'Endelea kuwa nasi mpaka mwisho kwa ushairi kamili hapo badae.
Mh. Aman mara baada ya kukabidhi zawadi yake ,anampongeza Mstaafu Mwalimu Bishanga
Mwanadada Hope mara baada ya kukabidhi zawadi yake kwa mstaafu
Mzee Mshashu akikabidhi zawadi yake
Walimu wa Shule ya Msingi Kashai wakiwa na zawadi yao
Bi Angel akiongea kama muweka hazina wa kamati ya maandalizi
Athman na Murshid wakifanya mawasiliano
Wanafamilia wakishusha bonge laburudani
Burudani kutoka kwa wanafamilia ikiendelea.
Sehemu ya Waalikwa wakipata msosi
Utaratibu wa kupata huduma ya Chakula ukiendelea..
Ndugu Athmani Bahati akipati mulo safi.
Taswira mbalimbali mapema kabla ya sherehe ya kumpongeza Mwl-Martha Bishanga kuanza.
Wakati Bi Husna Khaldi anaingia Ukumbini
Wakati familia ya Mama Seleda ikiingia Ukumbini
Mwanzoni wakiingia Ukumbini walimu wa Shule ya Sekondari Kashai
Upande wa Mapokezi mambo yalikuwa hivi
Ni mwendo kwa Kula kunywa na kufurahi
Bi Shatifa anasema: Safi sana..imekaa vizuri!
Dada Angel akiwajibika
KUFIKIA HAPA NIKWAMBA:BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
Picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu
KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA 2oo INGIA HAPA>>Bukobawadau Entertainment Media