HALMASHAURI MKOA KAGERA ZAAGIZWA KUTOTOA TENDA KWA WAKANDARASI WASIO NA SIFA
Serikali mkoani Kagera imeziagiza halmashauri zote za mkoa huo
kuzingatia sifa za wakandarasi wanao omba tenda za kujenga barabara
nakuwataka wakurugenzi wa halmashauri kutowakabidhi tenda za kazi
wakandarasi wasio na sifa wanao jenga barabara chini ya kiwango na
kusababisha adha kubwa kwa watumiaji wa barabara hizo.
Akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika mjini
Bukoba mbunge wa Bukoba vijijini Jonson Rweikiza amesema hakuna haja ya
kuwakabidhi wakandarasi wasio na sifa katika kujenga barabara na
nakuwataka wakurugenzi wa halmashauri kuzingatia vigezo na sifa za
wakandarasi hao wakati wa kugawa zabuni ili kupunguza adha zinazo
zijitokeza mara kwa mara na kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa madaraja
ambayo yamekuwa yakitole ahadi za muda mrefu bila kukamilika.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kagera Johni Mongera amesema
atafuaatilia kimalifu suala la ujenzi wa miradi mbalimbali inayoibuliwa
katika mkoa huo zikiwemo barabara na akaongeza kuwa halshauri sasa
zinatakiwa kushirikina na wakala wa babara nchini Tanrods na kuhakikisha
barabara zinajengwa kwakiwango kinachotakiwa ilikupunguza kero na
changamoto zinazo wakabili watumiaji wa barabara.
Hali hii imejitokeza kutokana na kuwepo kwa barabara nyingi na
madaraja yaliyojengwa chini ya kiwango likiwemo daraja la mtoto kanoni
ambalolinadaiwa limejengwa chini ya kiwango.