MKURUGENZI AMTIMUA MWANDISHI WA HABARI
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg. Cornel Ngudungi (mwenye miwani) akiwa katika moja ya mikutano yake.
Mwanahabari wa Radio na magazeti Mkoani Kagera Shaaban Ndyamukama katika kuwajibika
Mwanahabari wa Radio na magazeti Mkoani Kagera Shaaban Ndyamukama katika kuwajibika
NGARA.
Wakati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya
Kikwete akisisitiza watendaji wa serikali kufanya kazi na vyombo vya habari hali
imekuwa tofauti kwa baadhi yao na kulazimika kuwatimua wanahabari kwenye ofisi
zao
Hali hiyo imejitokeza jana wilayani Ngara mkoani Kagera ambapo Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya hiyo Cornel
Ngudungi alipomfukuza mwandishi wa
habari Shaaban Ndyamukama aliyetaka
kujua maendeleo ya kampeni za uchaguzi
Ngundungi ametoa kauli hiyo ofisini kwake
muda mfupi baada ya kumfukuza mwandishi huyo kwa madai kuwa anaandika habari
za kuichafua halmashauri
ya wilaya hiyo na kukiuka maadili ya uandishi
Mkurugenzi huyo amesema haoni umuhimu wa kutumia vyombo vya habari kutoa taarifa za maendeleo kwa wananchi kwa madai kuwa yeye hataki kuandikwa wala kutangazwa kwenye
vyombo vya habari
Ngudungi amesema
haoni haja ya kufanya kazi na
vyombo vya habari kwa sababu baadhi ya
waandishi wanapotosha jamii kwa kuripoti taarifa zisizo sahihi hali
ambayo inapelekea kulaumiwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa
“Nilitumwa kufanya kazi za wananchi sio na waandishi
wa habari wananchi wakishaona ninawafanyia nini inatosha” aliongeza mwandishi
anayepewa habari na kuiandika kinyume na jinsi alivyopewa siwezi kushirikiana
naye” Alisema
Akizungumza na wanahabari wenzake nje ya ofisi ya
mkurugenzi huyo mwandishi huyo amesema alifika kutaka kujua idadi ya vituo
vitakavyoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa wilayani humo na jinsi kampeni
zilivyo na changamoto zake
Ndyamukama amesema kwa kuzingatia na kufuata misingi ya Katiba, sheria, kanuni na taratibu wananchi wanayo haki ya kupata habari kupitia chombo chochote cha habari kama vile Radio Magazeti na Luninga
Ndyamukama amesema kwa kuzingatia na kufuata misingi ya Katiba, sheria, kanuni na taratibu wananchi wanayo haki ya kupata habari kupitia chombo chochote cha habari kama vile Radio Magazeti na Luninga
Imedaiwa kuwa mwanahabari huyo aliandika taarifa za
mmoja wa wafanyakazi kazi wa kituo cha Afya cha Lukole aliyetuhumiwa kuwapiga wagonjwa na kwamba taarifa hizo zilikuwa bado
kuhakikiwa na mkurugenzi huyo
Hata hivyo mkuu wa mkuu wa wilaya ya Ngara
Costantine Kanyasu amelaani kitendo hicho cha mwanahabari kufukuzwa akitafuta
taariza za maendeleo ya wananchi na kudai kuwa atafuatilia kujiridhisha ili
hatua zichukuliwe
“Kama hali hiyo imejitokeza badi mkurugenzi
anahitaji kuelimishwa kwani wananchi wana haki ya kupewa taarifa za maendeleo
ya halmashauri na masuala mengfineyo kwenye wilaya yao” Alisema Kanyasu
Pamoja na hayo imefahamika kuwa baadhi ya watendaji
wa kata na vijiji wakiwemo wakuu wa idara hawana mamlaka ya kutoa taarifa za
maendeleo kwenye vitengo vyao na kusababisha baadhi yao kulalamikiwa na
wananchi.
Wilaya ya
Ngara inavyo vijiji 75 vyenye vitongoji
394 vitakavyotumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa na idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni 133,317 sawa na 134%
kati ya walengwa 99, 259
kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 .