MKUU MPYA WA MKOA WA KAGERA AJITAMBULISHA WILAYANI NA KUKAGUA UJENZI WA MAABARA PAMOJA MIRADI YA MAENDELEO
Mkuu wa Mkoa wa Kagera John
Mongella atembelea Halamashauri za Wilaya za Mkoa wa Kagera kujitambulisha kwa Madiwani, Watendaji wa halmashauri za Wilaya pamoja na wadau mbalimbali wa
maendeleo ikiwa ni pamojana kukagua ujenzi wa maabara katika shule zote za
serikali.
Ziara hiyo ilianza Desemba 4,
2014 katika Wilaya ya Missenyi na
kufuatiwa Wilaya za Muleba Kyerwa, Karagwe, Ngara na Biharamulo. Mkuu wa Mkoa
John Mongella alitumia nafasi hiyo kuijimbulisha pia kutoa ufafanunuzi wa
majukumu makuu na muhimu ya mkuu wa mkoa katika nafasi yake.
Majukumu hayo ni pamoja na
kusimamia shughuli zote za maendeleo katika mkoa, kusimamia ulinzi na usalama
katika mkoa na jukumu la tatu ni kusimamia utii wa sheria katika mkoa. Katika
mikutano aliyoifanya na wadau na watendaji wa Halmashauri aliyatolea ufafanuzi
kwa ufasaha majukumu yake.
Katika kutekeleza majuku yake
mkuu huyo wa mkoa alifafanua zaidi juu
ya uwajibikaji wa watendaji wa serikali kwa kutumia mfumo uliopo kutoa huduma za jamii na kutekeleza miradi ya
maendeleo katika Halmashauri za Wilaya kwa kila mtendaji kuwajibika katika
nafasi yake ya kazi aliopo.
John Mongella alitoa onyo kali kwa watendaji wa Halmashauri
ambao hawatimizi wajibu wao wa kwenda
vijijini kufuatilia maendeleo ya wananchi, alisema atakikisha
anawachukulia hatua kali pale itakapobainika kuwa kazi yao ni kushinda ofisini
bila kwenda kwa wananchi.
Aidha alitoa maelekezo kwa
watendaji wa kata na madiwani kuwa na
siku maalum za kwenda katika halmashauri zao na siyo kila siku kushinda katika
ofisi za Wakurugenzi na kufanya kazi za wataalamu. Pia aliwaagiza Wakurugenzi
watendaji wa Halmashauri nao kutenga siku za kukukaa ofisini na siku za kwenda
vijijini kufuatilia miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya ofisi zao.
Ujenzi wa Maabara: Mkuu wa Mkoa John Mongella pia alitembelea na
kukagua ujenzi wa maabara tatu kila shule ya serikali unavyotekelezwa mkoani
Kagera ambapo mwisho wa kukabidhi maabara hizo ulikuwa Desemba 9, 2014
kulingana na agizo la Rais Jakaya Kikwete la mwaka jana Februari 2013.
Katika Halmashauri za Wilaya za
Missenyi, Muleba, Kyerwa, Karagwe, Ngara na Biharamulo ujenzi wa maabara katika
shule zote za serikali unaendelea ambapo vyumba
vitatu vya masomo ya Fizikia, Kemia na Biologia vinaendelea kukamilishwa
ikiwa ni pamoja na miundombinu ya maji na gesi ndani yake.
Mkuu wa mkoa John Mongella pamoja
na kukuagua na kupima na kuhakikisha maabara hizo zinajengwa kwa kufuata michoro
ya serikali pia alikuwa akijihakikishia kama vipimo vinafuatwa na kila kitu
kinachooneshwa kwenye ramani za majengo hayo kimewekwa kama ramani inavyoonesha, aidha aliagiza ifikapo January 2015 kila
maabara iwe imekamilika tayari kwa wanafunzi kuzitumia maabara hizo.
Miradi ya Maji: Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kagera John
Mongella hakusita kukagua miradi ya maendeleo ambayo imeshindwa kukamilika kwa
mwakati hususani miradi ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
ya vijiji 10 na miradi ya Quick win katika vijiji vinne vya Kamachumu,
Izigo, Rwanda na Itoju.
Katika miradi hiyo ambayo tayari
serikali imetoa mamilioni ya fedha imeshindwa kukamilika kwa wakati na kupelekea wananchi katika maeneo
hayo kuendelea kupata adha ya maji jambao ambalo lilimfanya Mkuu huyo Mkoa
kuwaagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi na kumpelekea taarifa baadaya wiki mbili.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya
Ngara Mkuu wa Mkoa John Mongella alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
kuhakikisha mradi wa maji wa Ngara mjini unakamilika na kufanya kazi ifikapo Januari 30, 2015 mara baada ya kugundua kuwa
tayari milioni 30 zilitumika ndivyo sivyo.
Aidha alimwagiza mweka hazina wa
halmashauri hiyo kuhakikisha mapato ya ndani ya mwezi Desemba 2014 yanaelekezwa
katika mradi huo ili huduma ya maji ipatikane haraka katika mji wa Ngara. Pia
Mkurugenzi wa halmashauri ya Ngara kuhakikisha anasimamia kesi ya ubadhilifu wa
milioni 30 ili mhusika awajibishwe kisheria.