NECTA YATANGAZA MFUMO MPYA
Dodoma. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limeanza mfumo mpya
wa kupanga matokeo ya kidato cha nne mwaka huu na ya kidato cha sita
mwakani, ambapo sasa madaraja yatapangwa kwa wastani wa pointi (GPA)
badala ya jumla ya pointi.
Hayo yalisemwa jana na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk. Charles Msonde katika mkutano wa wadau wa kampeni ya elimu kwa watoto wa kike walio katika mazingira magumu (Camfed).
Hayo yalisemwa jana na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk. Charles Msonde katika mkutano wa wadau wa kampeni ya elimu kwa watoto wa kike walio katika mazingira magumu (Camfed).
Dk Msonde alikuwa akitoa mada kuhusu uwekaji alama za ufaulu unaotekelezwa na Necta.
Alisema mfumo huo siyo mpya kutumiwa na Necta kwa
sababu umekuwa ukitumiwa katika kupanga matokeo ya wanafunzi wa vyuo vya
walimu.
“Mfumo utakaotumika kupanga madaraja ya mitihani
kwa wanafunzi wa kidato cha nne wa mwaka huu na kidato cha sita mwakani
na kuendelea utakuwa si ule wa kutumia jumla ya pointi badala yake
utakuwa ni wastani wa pointi,” alisema na kuongeza:
“Utaratibu huu siyo kwamba ni mpya kwa baraza la
mitihani, tumefanya hivyo kwa matokeo ya ualimu na hata tunapopanga
shule bora tumekuwa tukitumia GPA... Hatubadilishi thamani ya madaraja.”
Alisema kuwa thamani ya madaraja itabaki kuwa ni ile ile bali sasa watakuwa na mfumo unaolingana na kupanga matokeo ya ualimu.
Dk Msonde alisema lengo la kutumia mfumo huo ni kuwezesha kuwa na mfumo unaofanana katika ngazi zote za elimu nchini.
“Lengo jingine ni kuwarahisishia wenzetu wa TCU na
Necta na wadahili wengine wawe wanatumia mfumo unaofanana na wa kwetu
wasianze tena kubadilisha vyeti,”alisema.
Alisema lengo lingine ni kuelimisha Watanzania kuhusu mfumo huo mpya wa upangaji wa matokeo.
ya mtihani ambapo kwa kutumia mfumo wa jumla ya pointi ilikuwa ni vigumu kuuelewa.
Dk. Msonde alisema kwa mfumo wa kutumia jumla ya
pointi watanzania wengi walikuwa wanafikiri mtu akipata pointi nyingi
ndio amefaulu zaidi ya wale waliopata pointi chache.
Alisema tayari wametoa mafunzo ya uelewa juu ya mfumo huo kwa wadau mbalimbali wa elimu na kwamba wanautambua.
MWANANCHI
Alisema tayari wametoa mafunzo ya uelewa juu ya mfumo huo kwa wadau mbalimbali wa elimu na kwamba wanautambua.
MWANANCHI