NI DIAMOND NA WEMA NDANI YA TUZO ZA SWAHILI FASHION
MWANAMUZIKI wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Nasib Abdul,
Diamond Platinum anashindana na aliekuwa
mpenzi wake Wema Sepetu katika kuwania Tuzo ya Mtu mwenye ushawishi mkubwa
katika mitindo.
Tuzo hiyo zitatolewa kwenye Onesho la Mavazi la Swahili
Fashion 2014 linaloandaliwa na Kampuni ya 361 Degrees na zitatolewa siku ya
mwisho katika onesho la Swahili Fashion Week litakaloanza Desemba 5 hadi 7
mwaka huu