Bukobawadau

RIHANNA AAJIRIWA NA KAMPUNI YA PUMA

Msanii wa muziki nchini Marekani Rihanna anajiandaa kuanza kufanya kazi katika kampuni ya michezo Puma.
Ametangazwa kuwa mkurugenzi wa ubunifu wa vifaa vya kike na atakuwa uso wa vifaa vya mazoezi vya wanawake.
Rihana mwenye umri wa miaka 26 ataunda aina ya nguo zilizopo pamoja na viatu na kusaidia kubuni muundo mpya wa chapa cha bidhaa hizo.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo,Rihana amesema anafurahi kuona ni nini yeye na Puma wanaweza kubuni.
Wakuu wa kampuni ya Puma wanasema kuwa Rihana ataleta ubunifu katika ulimwengu wa riadha.
Nguo hizo mpya zitakuwa na mtindo wenye lengo la kuwaimarisha wanawake katika mazoezi mbali na kuwafanya kuamini miili yao pamoja na wao wenyewe.
Jukumu la Rihana litakuwa kuwa na ushawishi katika bidhaa zitakazoundwa pamoja na kuandaa ukuzaji wa bidhaa mpya.
Akiwa miongoni mwa kampeni ya Forever faster msanii huyo atashirikishwa na wanariadha kama viule Usain Bolt na Sergio Aguero.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bjorn Gulden amesema kuwa waliamua kumtafuta mshirika katika nguo za wanawake za kufanyia mazoezi kutokana na ushawishi mkubwa wa kampuni hiyo katika soka,riadha na mashindano ya magari.
Tunafurahi kumpata Rihana na tunajianda kuona ni nini tunaweza buni kwa ushirikiano wake.
Rihana si mtu wa kwanza nje ya michezo kujiunga na kampuni ya Puma.
Msanii 50 cent na Jay Z walitoa viatu na kampuni ya Reebok, huku Kim Kardashian akiwa uso wa viatu vya Sketchers na mumewe Kanye West akifanya kazi na Nike pamoja na Adidas.
Next Post Previous Post
Bukobawadau