Bukobawadau

CHADEMA Yalaani kufukuzwa Chuoni Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimelaani vikali uongozi wa Chuo kikuu cha Dodoma kwa kumfukuza chuoni mtetezi mkuu wa wanafunzi ambaye ndiye waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Philipo Mwakibinga.
Taarifa kutoka ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini zinasema viongozi wakuu wa chama hicho wanalaani tabia ya kufukuza ovyo viongozi wa serikali za wanafunzi ili kuwaziba mdomo.
Philipo Mwakibinga ni mwanachama machachari wa Chadema na aliwahi kugombea Uenyekiti wa Bavicha Taifa.
Inaaminika Mwakibinga amefukuzwa kwa sababu ya Itikadi yake kisiasa.Na haya ni maelekezo ya uongozi wa CCM mkoa wa Dodoma kwa viongozi wa chuo hicho wakiamini kufanya hivi ni kuwatisha wanavyuo wasijiunge na Chadema.
Taarifa zaidi zinasema Kiongozi wa upinzani bungeni Freeman Mbowe amemeiagiza wizara ya Elimu kipitia Waziri Kivuli Suzane Lyimo kufuatilia kwa ukaribu suala hili ili kulinda haki za wanachuo hawa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau