CHUKUA SOMO WALA USIJIBWETEKE!
Hatakama amekuahidi kila ulichowahi
kutamani, hatakama amejitambulisha kwa ndugu zako wote, hata kama wazazi
wako wamemkubali, hata kama ana vigezo vyote vya mume uliyewahi
kumdhania au kumuota, hatakama amekwisha kuvisha pete ya uchumba na hata
kama mmeanza maandalizi ya ndoa, fahamu kwamba kama tabia zako bado
haziendani na tabia za mke ingawa wewe ni mwanamke bado anaweza
akaahirisha mpango wakuoana na wewe bila kujali mmefikia wapi. Usisahau
kwamba sio kila mwanamke anatabia za
mke, ingawa kila mke ni mwanamke. Wanaume wanafahamu pakuoa, na nani
anastahili kuwa mke, na nani hastahili, ingawa wanaweza kukudanganya kwa
kila neno tamu ila ukweli wanao wenyewe moyoni kwamba huyu ni
wakupumzikia tu, na yule ni wakuoa, kwani haujawahi kwenda kwenye harusi
ya kijana mliyedhani atamuoa flani lakini siku hiyo mnona kamuoa mtu
mwingine na wala hamumfahamu anakotokea wala walikokutana? Au umesahau
kwamba kila mchezaji ana nguo za mazoezi na za mechi? Sasa jiulize wewe
ni wamazoezi au wewe ni wa mechi, akili mukichwa, badili tabia, ishi na
kuwa kama mke sio tu mwanamke, lasivyo utaishia kuwa “maid”, au “matron”
au msindikizaji na mhudhuriaji wa harusi za wenzako – Chris Mauki