IJUE HALI YA UCHUMI WA MKOA WA KAGERA ILIVYOKUWA KUFIKIA JUNI 2014 KUTOKANA NA UCHAMBUZI WA BENKI KUU YA TANZANIA
Pato la mkoa wa KAGERA (kwa bei za soko) lilikua kwa
asilimia 18.9 katika mwaka 2013 kufikia TZS 2.1 trillion kutoka TZS 1.8
trillion mwaka 2012. Pato la mkoa wa Mwanza limeongezeka kwa 21.9% kufikia TZS
4,987,176 mwaka 2013 kutoka 4,090,594 mwaka 2012. Kukua kwa pato hili
kulitokana na kupanuka kwa shughuli za kiuchumi hasa katika Kilimo, Mifugo na
Viwanda.
Mchango wa kila mkoa
kwa Pato la Taifa kwa Kanda ya Ziwa unaonesha kuwa mkoa wa KAGERA uko katika
nafasi ya 3 kwa kuchangia asilimia 15.3 ya pato lote la Kanda ya Ziwa. Mwanza
inaongoza kwa kuchangia asilimia 36.2, Shinyanga 22.9, Mara 14.3 na Kigoma
11.2. Wastani wa Pato la Mwananchi/Mkazi kwa Mkoa wa Kagera ni TZS 718,901 kwa
mwaka 2012/13.
Hali ya Mfumuko
wa Bei
Mfumuko wa bei kwa kanda ya ziwa (The Zonal headline
inflation) pamoja na mkoa wa Kagera kwa mwaka ulioishia mwezi June 2014 ULIANGUKA
kufikia asilimia 3.9% kutoka asilimia 5.5% za mwaka
uliotangulia. Hii ilitokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za chakula.
Wastani wa Mfumuko wa bei kwa kanda ya ziwa ulikuwa chini ya mfumuko wa bei wa
taifa uliokuwa ni asilimia 6.4.
Hali ya Upatikanaji wa Chakula
Kituo cha Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) cha Shinyanga
kilipokea mahindi tani 24,777.5 mwaka huu wa 2014 ikilinganishwa na tani 30,
700.9 zilizopokelewa mwaka jana 2013. Kituo kilisambaza tani 17,515.5 za msaada
wa mahindi (kwa bei nafuu) kwenye maeneo yaliyokuwa na uhaba wa chakula
ikilinganishwa na tani 31,079.8 kwa mwaka uluiopita 2013, hivyo kubakiza tani
7,989.8 ghalani kulinganisha na tani 727.8 tu kwa mwaka uliopita.
Uzalishaji wa Mazao ya Chakula – Kagera
Mkoa wa Kagera unaongoza kwa kuzalisha wastani wa tani 2,508,180
ya mazao ya chakula kwa mwaka, sawa na asilimia 33.9 ya mazao yote ya chakula
kwa Kanda ya Ziwa. Zao la ndizi ndilo linalolimwa zaidi kwa takriban nusu ya
mazao yote ya chakula katika mkoa wa Kagera – wastani wa tani 1,338,970.
Hata hivyo, kwa miaka ya karibuni, zao hili lilikumbwa na
ugonjwa wa nyanjano ambao umeathiri kiasi cha uzalishaji kwa mwaka. Mkoa
uko katika juhudi za kupambana na ugonjwa huu.
SEKTA YA KILIMO:
Ununuzi wa Mazao ya Biashara: KAHAWA
Ununuzi wa Mazao ya Biashara: KAHAWA
Mazao ya biashara kwa
mkoa wa Kagera ni pamoja na KAHAWA, CHAI NA MIWA YA SUKARI. KAHAWA ndilo zao
maarufu zaidi la biashara kwa mkoa wa Kagera. Kiwango cha ununuzi zao la KAHAWA
mkoani Kagera ilishuka kwa asilimia 27.0 kufikia tani 49,214 mwaka 2013/14
kutoka tani 67,415 zilizonunuliwa mwaka 2012/13. Kuanguka kwa kahawa kulitokana
na tabia ya zao hili kupungua kwa vipindi vya mizunguko ya misimu (cyclical
nature), pamoja na kuvushwa kwa kahawa kwa magendo kupelekwa nchi jirani.
SEKTA YA MIFUGO:
Idadi ya Mifugo Kanda ya Ziwa (Mkoa wa Kagera)
Idadi ya Mifugo Kanda ya Ziwa (Mkoa wa Kagera)
Katika Kanda ya Ziwa, shughuli za Ufugaji zinashika nafasi
ya pili baada ya kilimo. Na Kanda ya Ziwa ina wastani wa 42% ya mifugo yote
nchini. Katika mwaka ulioishia June 2014, thamani ya mifugo iliyouzwa kupitia
masoko/minada rasmi ilipungua kidogo kwa asilimia 1.6 kufikia TZS 201.1 billion
kulinganisha na TZS 204.3 billion katika mwaka uliotangulia, Ingawa idadi ya
ng’ombe waliouzwa iliongezeka kidogo kwa asilimia 0.7
Kushuka kwa thamani ya mauzo ya mifugo kulichangiwa na
kushuka idadi ya ng’ombe waliouzwa kwa asilimia 2.0 (kutokana na hali nzuri ya
chakula). Wastani wa bei ya Ng’ombe ilishuka kwa asilimia 2.1 hadi TZS
385,700.0 mwaka 2013/14 kutoka TZS 393,863.0 mwaka 2011/12.
SEKTA YA UVUVI – KANDA YA ZIWA
Kanda ya
Ziwa inachangia asilimia 80 ya ununuzi na usafirishaji nje wa bidhaa za samaki
nchini.
Ununuzi wa
samaki (sangara) kwenda viwanda vya samaki ulishuka kwa asilimia 31.0 hadi
kufikia tani 30,193.0 mwaka 2014 kutoka tani 43,773.5 zilizonunuliwa mwaka
ulioishia June 2013. (Halikadhalika Export zilianguka kwa 31% kufikia tani
14,923.4 mwaka 2014 kutoka tani 21,711.1 mwaka 2013. Hii ilitokana na uhaba wa
samaki wabichi waliofikishwa katika maeneo/mialo ya manunuzi.
Upungufu
huu mkubwa wa samaki unatokana na upungufu wa samaki wanaovuliwa ambao nao unatokana
na uzalishaji/uzalianaji mdogo wa samaki ziwani. Hii imechangiwa kwa kiasi
kikubwa na shughuli za uvuvi zisizoratibiwa (over fishing), uharibifu wa
mazingira na maeneo ya mazalia ya samaki na matumizi ya zana haramu za uvuvi.
Zana hafifu za uvuvi.
MAPATO YA NDANI NA FORODHA
Makusanyo ya mapato katika mwaka 2013/14 katika mkoa wa
KAGERA yaliongezeka kwa asilimia 6.54 kufikia TZS 27.56 billion kutoka TZS
25.87 billion mwaka 2012/13. Hata hivyo mapato haya yalikuwa chini ya lengo la
TZS 41,615.1
Mabenki ya Biashara – Mkoa wa Kagera
Kwa taarifa tulizonazo, tuna matawi 13 ya mabenki mbalimbali
hapa mkoani. Zote zikiwa na jumla ya Amana (deposits) zipatazo TZS 122.6
Billion na zikitoa ajira kwa wananchi wa Kagera 177. Pia kufikia mwezi June,
2014 Mkoa wa Kagera ulikuwa na Vyama vya Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) 129,
zikiwa na Wanachama 60,297 na jumla ya hisa TZS 821,762.