JAMBO BUKOBA KUENDESHA BONANZA LA MICHEZO KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI KAGERA 30 JANUARI, 2015
Jambo Bukoba ni Shirika
lisilokuwa la Serikali linalofanya kazi mkoani Kagera kwa kushirikiana na
serikali ya mkoa. Mwanzilishi wa Jambo Bukoba anaitwa Bw. Clemence Mlokozi ambaye asili yake
ni mkoani Kagera katika Wilaya ya Missenyi Kijiji Ishozi na anaishi nchini
Ujerumani.
Jambo Bukoba katika kuhakikisha inapunguza unyanyapaa wa kuwatenga watoto wa kike katika jamii imeweza kueneza elimu kupitia michezo kwa watoto wote kushirikiana kwa pamoja bila kujali jinsia za watoto iwe katika masomo , michezo au katika shughuli nyingine za kijamii.
Ili kuleta umoja katika mkoa kwa
watoto wa kike na kiume Jambo Bukoba kuanzia mwaka 2012 ilianzisha bonanza la
michezo kila mwisho wa mwaka la kuwaunganisha watoto kutoka shule mbalimbali
mkoani Kagera ili waweze kushirikiana pamoja kimichezo na kujenga kujiamini kwa
pamoja.
Bonanza la michezo la Jambo
Bukoba mwaka 2014 litafanyika mwaka huu 30 Januari, 2015 na kushirikisha Wilaya
zote za mkoa wa Kagera pamoja na
mwanzilishi wa Jambo Bukoba akiambatana na wenzake kutoka nchini Ujerumani.
Bonanza la michezo la Jambo Bukoba litafanyika katika viwanja vya Gymkhana Manispaa ya
Bukoba kuanzia saa 2:00 asubuhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ikishirikiana
shirika la Jambo Bukoba wanawakaribisha wananchi wote kuhudhuria na kushiriki
katika bonanza hilo.
Shirika la Jambo Bukoba chini ya
mwanzilishi wake Bw. Mulokozi tangu kuanzishwa kwake mkoani Kagera limekuwa likiwafunza watoto katika shule za msingi kila wilaya michezo midogo midogo ya kujenga
ushirikiano wa pamoja hasa watoto wa kike kujiamini na kushirikiana zaidi na wenzao wa kiume.
Jambo Bukoba katika kuhakikisha inapunguza unyanyapaa wa kuwatenga watoto wa kike katika jamii imeweza kueneza elimu kupitia michezo kwa watoto wote kushirikiana kwa pamoja bila kujali jinsia za watoto iwe katika masomo , michezo au katika shughuli nyingine za kijamii.
Shirika hilo pia hutoa vifaa vya
michezo kama vile fulana na bukta za michezo, viatu na mipira katika shule mbalimbali mkoani Kagera. Vilevile
ili kuhakikisha watoto wanaendelea kupata elimu nzuri Jambo Bukoba imeanza kukarabati
miundombinu mbalimbali katika baadhi ya shule za msingi mkoani hapa.
Miundombinu hiyo ni pamoja na madarasa
ambayo yameharibika na kuhitaji ukarabati, kujenga matundu ya vyoo vipya pamoja
na kukarabati ofisi za walimu ambazo ziko katika hali mbaya ili kuwarahisishia
walimu katika kutekeleza majukumu yao vizuri ya ufundishaji.
Lengo la mwanzilishi wa Jambo Bukoba Bw. Mulokozi
ni kupunguza kasi ya watoto wa kike kuanzisha mahusiano ya kimapenzi wakiwa
wadogo, pia kupunguza unyanyapaa wa
wtoto wa kiume kwa watoto wa kike ambapo Jambo Bukoba imepunguza tatizo hilo
kwa kiasi kikubwa mkoani Kagera.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014