MARUFUKU SHULE BINAFSI NCHINI KUWAFUKUZA WANAFUNZI WASIOFIKISHA WASTANI
Serikali imezipiga marufuku kitendo cha shule binafsi nchini
kuwafukuza ama kuwasitishia masomo wanafunzi wanaoshindwa kufikia
wastani na kwamba shule zote zitakazokiuka agizo hilo zitachukuliwa
hatua kali ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili huku ikiongeza kuwa
kuanzia mwaka 2016 itaanza kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi
kidato cha nne.
Onyo hilo la serikali kwa wamiliki wa shule binafsi za serikali
limetolewa na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi bungeni mjini Dodoma
katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 18 ulianza Dodoma katika kipindi
cha maswali na majibu kutokana na swali la msingi la Mh Conchesta
Rwamlaza ambapo waziri huyo amesema ni marufuku kwa mameneja na wamiliki
wa shule binafsi za sekondari kukaririsha, kuhamisha ama kuwafukuza
shule wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani wa shule husika kwa kuwa
kiwango cha ufaulu kilichowekwa na serikali ni wastani wa asilimia 30.
Aidha mbunge wa handeni Dr Henry Shekifu ameitaka serikali kutoa
tamko la lini itaanza kutoa elimu bila ya kuanzia elimu ya msingi hadi
kidato cha nne ili kuwawezesha watoto wote wa Tanzania kupata elimu
ambapo serikali imesema utekelezaji wake utaanza mwakani.
Awali kabla ya kuanza kwa shughuli za bunge spika wa bunge hilo Mh
Anne Makinda amemwapisha mwanasheria mkuu mpya wa serikali ndugu George
Mcheche Masaju.
Mara baada ya kuapishwa nje ya bunge akijibu swali la waandishi wa
habari kuhusu mswaada wa sheria ya mahakama ya kadhi ambao umeanza
kuibua mawazo kinzani kwa baadhi ya viongozi wa dini hasa wa kikristo
ndugu Masaju amesema wamepitia kwa umakini mswaada huo na kwamba hauna
athari zozote kwa mtu, vikundi vya dini na taifa kwa ujumla na
hautaingilia mambo yanaayosimamiwa na serikali ikiwemo makosa ya jinai
na taifa litaendeleaa kuwa wamoja.