MATUKIO KATIKA PICHA WILAYANI NGARA
LEO wafanyakazi na watumishi wa radio Kwizera kituo cha ngara
mkoani Kagera na Kigoma wamekutana na uongozi wa wa Radio hiyo luweka
mipango ya Pamoja kufanikisha utafutaji na utoaji habari kwa jamii
inakosikika radio hiyo hadi nchi jirani za maziwa makuu,
Pichani ni
watumishi wa Radio Kwizera Mkoani Kagera Kigoma na DRC wakiwa na
Mkurugenzi wa Radio Kwizera Fr Damas Misanga.
Mkurugenzi wa Radio Kwizera Fr Damas Misanga pichani amewataka wanahabari
katika vituo wanakofanyia kazi kuthamini
kwanza usalama wa maisha yao na kufuatilia habari baadaye kwani wanaweza kuwa
chambo cha na kupoteza maisha yao
Katika matukio makubwa yaliyoko mbele mwaka huu ya
uandikishaji wapiga kura katika daftari la wapiga kura , maoni ya kupitisha
katiba iliyopendekezwa, kampeni za uchaguzi mkuu hadi kuwapata madiwani wabunge
na Rais
Fr Damas Misanga kawataka wanahabari hao kuhakikisha
wanatoa habari ambazo sio za uchochezi
na kuwapa nafasi wanaolalamikiwa kutoa maoni yao bila kutumiwa na
wanasiasa kwa maslahi yao binafsi
Amesema kuwa habari nyingine lazima kabla ya
kufikishwa radioni kuwe na uchunguzi na kuhoji mamlaka husika ili kila mmoja
kupata haki yake kwa kukuza demokrasia na utawala bora
Mwezi Machi Kituo cha Radio Kwizera kina tarajia
kuenea kwa kupanua matangazo yake katika mikoa ya Kagera Mwanza Geita hadi wilaya
ya Kahama ikiwemo mikoa ya Rukwa na Katavi.
Watumishi wa Radio Kwizera Mkoani Kagera Kigoma na DRC wakiwa na
Mkurugenzi wa Radio Kwizera Fr Damas Misanga katika picha ya Pamoja
Habari na picha By Shaaban Ndyamukama