PROF.IBRAHIM LIPUMBA APANDISHWA KIZIMBANI
Mwenyekiti wa CUF amepandikishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amepandikishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu
Jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shtaka moja ya kuwashawishi wafuasi wa chama chake kufanya kosa la jinai.
Awali kabla ya kufikishwa katika mahakama hiyo Profesa Lipumba alifika katika kituo cha polisi ambapo alitakuwa kuripoti yeye na viongozi wengine wa chama hicho ambao walikamatwa katika tukio la maandamano na badaa ya kiongozi huyo kuzungumza na polisi aliruhusiwa kuondoka na ndipo alipozungumza na waandishi wa habari kulaani kilichofanywa na polisi.
Akisimulia namna alivyopata kipigo hadi kupasuka sehemu ya kichwani naibu mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho Bw Abdul Kambaya amesema anakumbuka silaha mbalimbali zilitumika ikiwemo spana na kufungua tairi ya gari ambayo ndio iliyomjeruhi kichwani

Wakati viongozi hao wa CUF wakiendelea kufanya mahojiani mbalimbali na
waandishi wa habari alikuja afisa mmoja wa polisi na kumwita profesa
Lipumba na kuondoka naye kuelekea katika moja ya ofisi zilizopo kituoni
hapo ambapo baada ya muda wa takribani saa moja na nusi hali ya kiongozi
huyo ilibadilika na kukimbizwa katika kituo cha afya cha umoja wa
mataifa kilichopo karibu na viwanja vya Leaders akiwa chini ya ulinzi
mkali wa jeshia polisi katika gari lenye namba za usajili Pt 2566 aina
ya rav 4.
Baada ya matibabu msafara wa polisi ulielekea katika
mahakama ya kisutu ambapo wakili wa serikali Joseph Maugo mbele ya
hakimu mkazi Mh Isaya Arufani aliiambia mahakama kuwa kati ya tarehe 22
na 27 jan mwaka huu akiwa kama kiongozi wa chama aliwashawishi wafuasi
wake kutenda kosa la jinai na kuongeza kuwa upelelezi haujakamilika na
hawana pingamizi na dhamana.
Upande wanasheria wanaomtetea Mh Lipumba wapo sita wakiongozwa na wakili Mohamedi Tibanyendela na Peter Kibatala ambapo
Waliomba mahakama itoe masharti mepesi ambapo Mh Lipumba yupo nje kwa dhamana ya watu wawili waliosaini bondi ya shilingi milioni mbili na shauri hilo litatajwa tena Feb 26 mwaka huu