Bukobawadau

RC JOHN MONGERA WILAYANI NGARA

Siku ya Jana Mkuu wa mkoa wa kagera John Mongela ametembelea mradi wa utafiti wa madini ya Nickel (Kabanga Nickel wilayani Ngara akiambatana na viongozi wa chama na serikali wilayani Ngara kutambua uwepo wa watafiti wa madini hayo na shughuli zao
 Katika ziara yake katika mradi huo yeye kama mwenye kiti wa ulinzi na usalama mkoani Kagera kapewa slaha ya kukabiliana na matukio ya usalama kutoka kwa kamanda wa ulinzi wa kabanga Nickel Lok Piun wa Nepal  kama ishara ya mahusiano mema kiusalama.
Matukio ya picha Mkuu wa mkoa wa kagera John Mongela alipotembelea mradi wa utafiti wa madini ya Nickel (Kabanga Nickel wilayani Ngara)
 Akiwa katika mji wa Rulenge wilayani Ngara Mongela amesema wananchi waunde vikundi hasa rika la vijana kupata mikopo toka serikalini na kuanzisha miradi ya ujasiliamali kwa kutumia umeme kwenye maeneo yao na kujiajiri
 Aidha katika wilaya ya  Biharamulo amewataka viongozi wa vijiji na kata kuepuka kupokea maagizo kutoka kwa wananchi walioko mikoani kutaka kufungiwa umeme kwenye maeneo yao tofauti na michoro ya njia za kupitisha nishati hiyo 
Mkuu wa wilaya ya Biharamulo Richard Mbeho akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera na viongozi wa chama na serikali wa wilaya ya  Ngara na Biharamulo mara baada ya mkuu wa mkoa kuwasili katika kata ya Nyakahura akitokea wilayani Ngara
Kabla ya kupata umeme wananchi wa Nyakanazi wilayani Biharamulo walitumia mashine za kusaga nafaka kuchaji betri za magari kwa ajili ya sghuli mbali mbali wakitumia wmwanga utokao kwenye betri hizo
Picha na  Nassib Shaaban
Next Post Previous Post
Bukobawadau