SAKATA LA ESCROW;Watumishi watatu wa serikali wapandishwa kizimbani.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru imewafikisha
mahakamani watumishi watatu wa serikali akiwemo mkurugenzi wa fedha wa
benki kuu ya Tanzania BOT Julius Angelo kwa tuhuma za kupokea rushwa ya
zaidi ya shilingi bilioni 1.8 ambazo ni sehemu ya fedha za Escrow.
Watuhumiwa hao wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi
kisutu,jijini Dar es Salaam ambapo mara baada ya kusomewa mashitaka yao
mahakama imetoa zuio la matumizi ya fedha hizo hadi pale kesi ya msingi
itakaposikilizwa na kutolewa hukumu na hilo limekuja baada ya upande wa
mashtaka kuiomba mahakama hiyo kutoa zuia hilo.
Mtuhumiwa wa kwanza ni Julius Angelo mkurugenzi wa fedha wa benki
kuu ya Tanzania BOT ambaye waendesha mashitaka kutoka Takukuru Leornad
Swai na Marx Ari wamedai mbele ya hakimu mkazi Devota Kisoka wa mahakama
hiyo kuwa Angelo anatuhumiwa kwa shtaka la kupokea rushwa ambapo
februari 06 mwaka jana, akiwa jengo la benki ya mkombozi alipokea sh.
Milioni 161.7 kupitia akaunti yake.
Waendesha mashitaka hao wameieleza mahakama kuwa Angelo alijipatia
fedha hizo kutoka kwa James Rugemalira ambaye ni mkurugenzi wa
Engineering and Marketing Ltd vip na ambaye pia alikuwa mkurugenzi wa
kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited IPTL, kama
tuzo ya kusaidia kuidhinisha malipo kutoka kwenye akaunti ya Tegeta
Escrow kwenda PAP.
Mtuhumiwa huyo amekana shitaka hilo na kutakiwa kuwa na wadhamini
wawili watumishi wa serikali watakaosaini bondi ya sh. Milioni 50 kila
mmoja na yeye kutakiwa kutoa sh milioni 80 taslim au mali isiyohamishika
yenye thamani ya fedha hizo masharti aliyoshindwa kutimiza na kupelekwa
rumande hadi januari 27 mwaka huu upande wa mashitaka utakapoanza kutoa
maelezo ya awal
Mshitakiwa mwingine ni Stephen Urassa ambaye ni mwanasheria wa
shirika la umeme nchini Tanesco ambaye mbele ya hakimu Janeth Karienda
waendesha mashitaka hao wa Takukuru wamedai kuwa mtuhumiwa huyo
anakabiliwa na kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh milioni 161.7 kwa
Rugemalira kama tuzo kwa kuiwakilisha Tanesco na kampuni nyingine
zilizokuwa zimeingia mkataba shirika hilo, yuko nje kwa dhamana hadi feb
11 mwaka huu baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Mtuhumiwa mwingine ni Kyabukoba Mutabingwa ambaye ni meneja
misamaha ya kodi TRA na anatuhumiwa kwa makosa manne ya kupokea rushwa
ya zaidi ya sh. Bilioni 1.4 ambapo alikuwa anaiwakilisha tra pamoja na
kampuni ya mabibo wine ambapo waendesha mashitaka hao wamedia mbele ya
hakimu Janeth kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo jan 27 mwaka jana
ambapo alipokea bilioni 1.6 mwezi huohuo milioni 161.7 na julai 15
alipokea sh milioni 161.7 novemba 14 alipokea sh milioni 161.7.
Aidha mtuhumiwa huyo ametakiwa kuwa na wadhamini watatu
wanaoaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya shilingi milioni 340 na
yeye atoe fedha taslim sh bilioni 1 na ameshindwa kutimiza masharti ya
dhamana na kupelekwa rumande hadi jan 29 mwaka huu kesi yake
itakapotajwa tena kwa maelezo ya awali