Sugu anusurika kifo, apata ajali mlima Kitonga
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amenusu kifo baada
ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali katika eneo la mlima Kitonga
mkoani Iringa.
Taarifa za awali kutoka kwa katibu wake Kwame
Anangisye zimeeleza kuwa Mbunge huyo akiwa na watu wanne kwenye gari
yake alipata ajali hiyo mwanzoni mwa mlima Kitonga akitokea Mbeya
kuelekea jijini Dar es Salaam.
“Tulipoanza kushuka kwenye mlima Kitonga gari ya Mbunge ilifeli breki na kisha kupinduka mara moja na kugeukia ilikotokea, ilikuwa ajali mbaya lakini tunashukuru Mungu tumepona.
“Tulipoanza kushuka kwenye mlima Kitonga gari ya Mbunge ilifeli breki na kisha kupinduka mara moja na kugeukia ilikotokea, ilikuwa ajali mbaya lakini tunashukuru Mungu tumepona.
Amesema pamoja na ajali hiyo kuonekana mbaya
kwao, wanamshukuru Mungu kwani waliweza kutoka wakiwa salama na hakuna
hata mmoja aliyepata maumivu makali.