Uandikishaji Vitambulisho vya kura vipya kuanza Februari.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Dkt. Florens Turuka akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa
habari wa vyombo mbalimbali nchini, mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza la
Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo, mjini Dodoma.
(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Wajumbe wa
mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika mkutano
wa Baraza hilo leo, mjini Dodoma.
(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano
wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakisoma nyaraka za mkutano wa Baraza hilo leo, mjini Dodoma.
(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Wajumbe wa
mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakisoma nyaraka za mkutano wa Baraza hilo leo, mjini Dodoma.
(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Dkt. Florens Turuka (walio kaa mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja
na wajumbe wa Mkutano wa Baraza la
Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kufungua Mkutano huo, leo, mjini Dodoma.
(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Na. Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka
amesema kuwa Serikali inatarajia mwezi Februari mwaka huu kuanza uandikishaji na uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Wapigakura kwa kutumia
teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR) ili kuboresha Daftari la
Kudumu la Wapigakura ambapo maboresho hayo yatafuta matumizi ya vitambulisho
vya kupigia kura vya sasa.
Turuka alifafanua kuwa maboresho ya daftari hilo nchini yatafanyika kwa watu
wote wenye sifa za kupiga kura Oktoba mwaka huu na kukamilika kabla ya kura ya
maoni ya Katiba, katika kura ya
maoni ya Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu wa 2015, mpigakura atatumia kitambulisho
kipya atakachopatiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), baada ya kuandikishwa
upya katika mfumo huo.
Akiongea mara baada ya kufungua
Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo, mjini Dodoma, Turuka
alibainisha kuwa tayari serikali imefanikiwa kuifanyia
majaribio teknolojia hiyo ya BVR katika majimbo matatu ya hapa nchini ambayo
ni; Jimbo la Kawe – Dar es Salaam , Jimbo la Kilombero - Morogoro na Mlele - .
“Serikali
imefanikiwa kutekeleza kwa ufanisi
jaribio la teknolojia ya BVR japo ambapo
changamoto zilizo jitokeza katika majaribio hayo tayario tumeshazifanyia
kazi katika kuboesha zoezi hilo, hivyo napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa
teknolojia hiyo ya kisasa kuwa lengo la serikali la kutumia teknolojia hiyo ni
kumuwezesha mwananchi kujiandikisha kupiga kura kwa kutumia njia ya kisasa
hivyo nawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi wakati zoezi hilo litakapo anza kwani tunaandikisha wapigakura ”
alisistiza Turuka
BVR ni mfumo wa kuchukua taarifa za mtu za kibaiolojia hasa alama za vidolya e kwa ajili ya kuzihifadhi katika kanzidata (database) kwa ajili ya utambuzi. Mwaka 2004, NEC ilianzisha Daftari la Kudumu la Wapigakura ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa taarifa za wapigakura na uhifadhi wa taarifa za kielektroniki. Wapiga kura wa zamani kwa maana waliokuwa kwenye daftari la sasa watatakiwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha kuchukuliwa taarifa zao hasa za vidole, picha na saini zao katika mfumo mpya wa BVR na hatimaye kupewa vitambulisho vipya .
Mwisho.