Bukobawadau

UNAGOMBANA NA DILI?...HIZI SIO AKILI

Dah, kile kimvua cha juzi wanangu ilibaki hivi tu ...Kiduuuuchu nidedi kudadadeki, natoa hai kwa wanangu wote wa kitaa...mtu mzima niko fiti na magumashi yanasonga kama kawa...kama dawa na hivi ninavyokwambia, vere vere sun, Zee linakuwa hewani kupitia mdimuz.blogspot.com kuanzia mwezi ujao, ...sasa kuna jambo moja ntasisitiza.
Watu deile unaambiwa wanakomaa na SMS kwamba wamezimia mzigo wa Zee la Nyeti nini, ...Hapando’ ntawashtukia, kwamba ni kweli ni wana au siyo, maana watakuwa wanaipata ile laivu, au siyo? Najua wengine mtazingua, kwamba labda homu hakuna intaneti na swali litakuwa kwani huna android?
…Mambo ya longtaimu ambayo Zee kama Zee hayazimii kwa sana, nunua tu kitu cha android uweze kuwasiliana na Zee.
...Humu ndani nitakuwepo kama kawa ila nataka kuwazoesha kulipata Zee kila Jumatatu mtandaoni ili na wenzetu walioko mambele wapate chansi ya kunisoma, uongo? Mi mtu? ...mi Zee bwana.
Big Up kwa mwanangu Ally Tozzy, niligumiana naye mitaa ya kati mwanangu tulipiga naye mzigo longtaimu pale globo...alikuwa mtu wa kimya kimya mbaya unaambiwa ila juzi nimepandisha juu pale Kawe Ukwamani, nikamuona mtu mzima anasubuma tukutuku nini, maisha shwari...ile ile yaani.
Kitaani kwa mchizi wangu Karim Temba, pale Tegeta kuna ishu moja inaendelea, wana wawili unaambiwa wamenuniana kinoma, kisa demu, kwanza hii tusiiingilie maana utamu wa shori si wanaujua wenyewe bwana?
Mi naipotezea lakini kikubwa ni kwamba machizi walikuwa wanategemeana kweli kwenye michongo na kiukweli dili zao zikibumbuluka huwa ni mkwanja mrefu kinoma babu. Sasa wamezinguana, wako homu tu wamelikita na demu huenda muda simrefu akachukuliwa jumla na mchizi flani kutoka migodini.
Mnaionaje hii wanangu ndiyo nshaiweka mezani hivimtu mzima...
Mi imenizingua kimtindo, haukamz watoto wa kiume mnaacha dili usawa huu, dili za msingi mnanuniana kisa demu? Hata ingekuwa nini kudadadeki usawa huu unaambiwa hata kama mkizinguana kisa nini, likija suala la dili inabidi muweke bifu lenu pending, mnapiga mchongo kwanza, halafu mchongo ukipita fresh mnaendelea na kununiana kwenu au siyo mwanangu?
Au nuna halafu ubaki na njaa na ukinipiga mzinga sikupi
Hizi taimu wanangu ni mbaya kama mlikuwa hamjazishtukia, siyo taimu na kumaindiana kivile, hizi ndiyo taimu za kumeki. Na kuzinguana katika laifu ya kila siku hakueskepiki, huwezi kuepuka kumzingua mwanao, lazima itatokea tu wantaimu, umezingua, na hapo ikitokea basi na nyie ndiyo muanze kukomaaaaaaa...
Muwe wepesi kuambiana ukweli kwamba mwana...hapa nimezingua lakini sio ishu, tusonge, siyo kuanza kumaindiana na kunyimana michongo.
 ..Hailipi kiukweli
Na kama mmezinguana mpaka mnashindwa kumeki pisi bitwini, basi upigeni mchongo hata kama mmenuniana...umeona?
Itaneni pigeni mchongo huku unaambiwa nyuso zimejikunja ile ile kudadadeki, mchongo ukimalizika mnaenda kuchukua mchongo huku mnaongelea dili hilo tu, mkishagawana poa kila mtu anatambaa kivyake.
Lakini msije mkashindwa kumeki mane kwa sababu ya kiugomvi cha striti...Zee hapendi.
Mi nimeishia hapa kwa leo wanangu ninasisitiza wanangu nawapa taimu kuanzia leo mpaka Septemba moja muwe mshanunua redio za kisasa, siyo midude yenu hiyo, mtakuwa mnaninyaka deile na zile busara zilizokuwa kushoto hapa zitakuwa laivu kwa hewa, au siyo?
Sasa we bisha uone!
HENRY MDIMU
Next Post Previous Post
Bukobawadau