Bukobawadau

VIONGOZI NA WAFUASI WA CUF WATAWANYWA KWA MABOMU YA MACHOZI TEMEKE DSM

Jeshi la Polisi limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa chama cha wananchi CUF ambao walikuwa wanakwenda kushiri katika mkutano wa kuwakumbuka wanachama wenzao waliouwawa huko visiwani Zanzibar mwaka 2001 huku ikitumia nguvu kubwa kuwapiga waandishi wa habari waliokuwa wakitekeleza majukumu yao ambapo mwenyekiti wa taifa wa chama Profesa Ibrahim Lipumba na viongozi wengine wamejikuta wakipata kipigo na hatimaye kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi.
 Hali ya sintofahamu ilianzia katika ofisi CUF Temeke pale mwenyekii wao Profesa Lipumba alipowatangazia wafuasi hao kuwa hakutakuwepo na maandamano ya kuelekea katika viwanja wa Zakhem na badala yake atakwenda mwenyewe katika mkutano huo kuwatangazia wananchi ambao tayari walikuwa wameanza kukusanyika huko katika eneo la mkutano.
Baada ya tangazo hilo safari ikaanza na ndipo mvutano ukaanza baina ya polisi na viongozi wa CUF.
Baada ya mabishano na majadilino ya muda mrefusafari ikaanza tena kutokea Temeke kuelekea Zakhem.
Msafara huo ulipofika mtoni kwa azizi likatolewa agizo lingine la kusitishwa kwa msafara huo
Baada ya majadiliano hayo hali ya hewa ikabadilika temeke ikageuka kuwa iraq ndogo.
Baadhia ya mabomu yaliyokuwa yanarushwa yalidondoka katika makazi ya watu likiwemo darasa dogo la wanafunzi wenye umri usozidi miaka mitano ambapo walionekana wakitokwa machozi na makamasi huku mwalimu wao Bi Halima Semsela akidaia kuna watoto wengine hajui walipokimbilia
Next Post Previous Post
Bukobawadau