Bukobawadau

WATU 7 WAKAMATWA MAUAJI YA KASHAI

Marehemu Onesmo Charles Muta aliye uwawa kwa kupiwa risasa nyumbani kwake Katatorwansi Kashai
Jumla ya watu nane wanashuikiliwa na polisi mkoani Kagera, baada ya kusababisha mauaji kwa aina mbalimbali.
Kamanda wa polisi mkoani Kagera Enry Mwaibambe, amesema kuwa katika tukio la kwanza  wanamshikilia Burhan Issaya Tatuleka miaka 40 na mkewe Madina Hamis au mama Jamila miaka 35 wakaazi wa Rwinyama Bugarama Ngara, wakihusishwa na mauaji ya Alfaxad John au Hashim miaka 36 yaliyofanyika 14 jan 2015 saa 3 usiku.
Taarifa inasema kuwa marehemu aliuawa kwa kitu chenye ncha kali, wakati akiendesha pikipiki T 237 CDKakitokea kwenye majukumu yake ya kila siku, huku siku mbili kabla akiibiwa Mbuziwanne na watu aliowaona ila akaogopa kutoka nje, na akapokea ujumbe kutoka kwa mpenziwake ukimpa pole na kusema kuwa angetoka nje angeuawa.
Wakati huo huo Polisi inawashikilia watu 7 kuhusiana na mauaji ya Onesmo Charles Muta miaka 24 mkazi wa Katatorwansi Kashai manispaa ya Bukoba, ambapo tarehe 15 jan 2015 saa nane na nusu usiku, kundi la wahalifu zaidi ya 10 walivamia nyumba aliyokuwa anaishi marehemu na wapangaji wengine, wakaanza kuwapiga huku wakidai fedha wakiwa na mapanga na marungu na kumchoma marehemu na kitu chenye ncha kali kifuani na kufariki papo hapo huku wapangaji wengine wane wakijeruhiwa.
Kamanda Mwaibambe amewataja majeruhi kuwa ni Philipina Onesmo mke wa marehemu, Edwin Haipolite mfanyabiashara ndogondogo, Adelene Simon na Denice Gervas.
Amesema kuwa uchunguzi unaendelea huku watuhumiwa wakiendelea kushikiliwa na jeshi hilo.
Mazishi ya Onesmo Charles pichani hapo chini, yamefanyika kijijini kwao Gera Misenyi mkoani Kagera jioni ya Ijumaa Jan 16,2015
Next Post Previous Post
Bukobawadau