WAZAWA WA MKOA WA KAGERA WAISHIO NJE YA MKOA WAJIPANGA KUUREJESHA MKOA HUO KATIKA ENZI ZA NSHOMILE
Baada ya kilio cha muda mrefu kwa wazawa wa Mkoa wa Kagera ambao wanaishi nje ya mkoa huo na wasomi na
wenye uwezo mkubwa kiuchumi kukumbushwa kila mara kurudi nyumbani kuwekeza na
kuinua uchumi wa mkoa wao, wanakagera
hao sasa wameanza kuitikia wito huo kurudi nyumbani.
Wanakagera hao ambao wanaishi nje ya Kagera wameunda
umoja wao ambao unajulikana kama Friends of Bukoba na kuanza kuweka
mikakati ya kuukumbuka mkoa wa Kagera ambako ni kwa kwao ili uendane na sifa
yake kama ilivyokuwa miaka ya 1970.
Kutoka kila kona ya dunia Wanakagera sasa wameamka ili
kuurejeshea mkoa wa Kagera jina lake la NSHOMILE lakini kufuta nshomile
but no course, hayo yamebainika baada
ya wazawa wa Mkoa wa Kagera kupitia Friends of Bukoba kuanzisha mfuko wa maendeleo wa mkoa.
Wazawa wa Mkoa wa Kagera wakiongozwa na Mzee Kamzola kupitia
Friends of Bukoba wanasema kuwa tayari wamechangia shilingi milioni 500 na
kipaumbele chao ni Elimu kwanza ili kufuta ujinga katika kizazi cha sasa cha
mkoa wa Kagera na kuwa nshomile kama zamani.
Hayo yalibainika mara baada ya Siku Kuu za Mwisho wa mwaka
2014 zilizowakusanya Wanakagera wengi waliokuja kusherekehea na familia zao
Mkoani humo. Mapema Januari 2015 wanakagera hao walianza mikakati ya
kukutana na wanakagera wanaoishi ndani
ya Kagera kuweka mpangokazi wa pamoja.
Wakikutana na Mkuu wa Mkoa katika ofisi yake pamoja na wadau
wa maendeleo wa mkoa waliweka mikakati na kubainisha kuwa mkoa wa Kagera hapo
miaka ya 1970 ulipata umaarufu kwasababu ya elimu na kwa sasa elimu imeshuka
kwa kiwango kikubwa.
Wanakagera kupitia Friend of Bukoba walibaisha kuwa tayari
wao wameamua kuanza na elimu lakini wanawashirikisha wadau wengine waishio mkoani
hapa jinsi ya kukukuza kiwango cha elimu na uwekezaji katika Nyanja nyingine
utafuata baadae.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella alisema suala hilo
lazima liwashirikishe wadau wengi ili kusije tokea matatizo mbele ya safari.
Pia wananchi waishio ndani ya mkoa kuwa tayari kuchangia katika kuuendeleza
mkoa wao na si kuwategemea waishio nje ya mkoa pekee katika maendeleo.
Wito, wewe mzawa wa mkoa wa Kagera unakumbushwa kupakumbuka
nyumbani kwa maendeleo ya mkoa wako uweze kukua kiuchumi.