Bukobawadau

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI YATOA ELIMU JUU YA MTANGAMANO WA JUMUIYA KWA WANANCHI WA MKOA WA KAGERA

 Akina mama wajasiliamali wakiwa katika kikao
Bw. Amantius Msole Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Aiwa na Bw. Clement Ndyamukama Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba Katika Kikao na Wadau
Naibu Katibu Mkuu Bw. Amantius Msole Akiongea na Waandishi wa Habari Mkoani Kagera Mara Baada ya Kikao na Wadau.

Wataalam kutoka Wizara  ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa kiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amantius Msole wanatembelea mkoa wa Kagera kutoa elimu kwa wananchi juu ya utangamano wa jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuona juu ya uelewa wa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Pamoja na kutoa elimu hiyo wataalamu hao walitoa nafasi katika kikao kilichofanyika tarehe 24/01/2015 kwa wajasiliamali wadogo hasa akina mama kueleza changamoto mbalimbali wananzokumbana nazo katika kufanya shughuli zao za ujasiliamali hasa kutafuta masoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wataalam hao kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki walitoa mada juu maeneo makubwa matatu ambayo ni kuhusu Umoja wa Forodha, Maeneo ya msingi katika soko la pamoja, pia na masuala ya msingi kutekelezwa katika umoja wa fedha, aidha mafanikio ya mtangamano hadi sasa.

Baada ya kutoa mada hiyo wadau waliohudhuria kikao hicho hasa akina mama wajasiliamali walibainisha changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wakati wakitekeleza shughuli zao za ujasiliamali ambapo walisema kuwa hawajawa na uelewa wa kutosha jinsi ya kufanya biashara zao.

Changamoto nyingine walioibainisha ni kuwa wajasiliamali kutoka nchi za wananchama wana fursa za kufanya biashara zao bila kuwekewa vikwazo nchini kwetu, lakini watanzania wamekuwa wakipata vikwazo vingi pale wanapo jaribu kupenya na  kupeleka bidhaa zao katika nchi hizo kutafuta masoko.

Aidha kikwazo kingine ni kuhusu shirika la viwango Tanzania (TBS) kutotimiza wajibu wake hasa katika kuhakiki bidhaa za wajasiliamali na kutoa idhini na kutokuwa na ofisi katika mkoa ambapo imekuwa mojawapo ya kikwazo kikubwa kwa wajasiliamali kuzalisha bidhaa zenye viwango.

Pamoja na vikwazo hivyo beria nyingi katika njia ziendazo katika nchi wananchama zimekuwa zikiwakwaza wajasiliamali pia na kutokuwa na elimu juu ya kodi halali ambazo wanatakiwa kulipia kwa bidhaa wanazoshughulika nazo katika ujasiliamali wao.

Akitoa ufafanuzi juu ya changamoto hizo Naibu Katibu Mkuu Bw. Amantius Msole alisema kwa kushirikiana na wadau wengine mfano Wizara ya Viwanda na Biashara, TRA, na Shirika la Viwngo (TBS) watakaa pamoja na  kuona jinsi ya kutatua changamoto hizo ili kusiwepo na vikwazo visivyokuwa vya lazima.

Aidha Bw. Amantius alisema katika kukabiliana na changamoto hizo wizara yake imeamua  kutembelea mkoa wa Kagera na maeneo ya mipakani kama Mutukula, Mulongo, Rusumo na Kabanga ili kutoa elimu na kusikia changamoto zilizopo na kuangalia jinsi ya kuzitatua ili kuimarisha mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Next Post Previous Post
Bukobawadau