ASASI YANUIA KUPAMBANA NA UMASKINI KATA YA KANYIGO
NA MWANDISHI WETU,BUKOBAWADAU,Missenyi
KAMATI tendaji ya asasi ya Kupambana na umaskini katika jamii,katika kata ya Kanyigo Wilaya ya Missenyi iitwayo CONCERN FOR COMMUNITY
RESOURCES(CCRD) yenye makao yake katika Kijiji cha Bugombe,imefanya mkutano wake mkuu hivi karibuni kutathmini kazi ya mwaka uliopita na kuandaa mikakati ya mwaka huu 2016,itakayojadiliwa na mkutano mkuu wa wanachama wote.

Asasi hiyo iliyosajiliwa mwaka 2013 Agosti,imo kwenye mchakato wa kuhakikisha inawashirikisha wanachama na jamii kwa jumla,kutumia vizuri raslimali walizo nazo katika kujiletea maendeleo,badala ya kubweteka tu wakisubiri misaada ya serikali.
Katika mkutano huo,kamati imejihimiza kila mmoja kuhakikisha anatimiza majukumu yake,na kuwa lazima taarifa ya shughuli za asasi iwe ikitolewa kwa ngazi za kijiji,kata wilaya na taifa ili wadau waelewe kinachoendelea.

Pichani kutoka kushoto ni Mratibu na pia Katibu wa CCRD,Arbogast Mutayoba,na kulia ni Mwenyekiti wa asasi hiyo,Godwin Lutimba
Miongoni mwa shughuli za asasi hiyo ni kusaidia watoto yatima na walio katika mazingira magumu,kuhifadhi mazingira,elimu ya uraia na kilimo chenye tija.
Picha na Mutayoba Arbogast