HII INAHUSU KWA JUMAMOSI YA LEO FEB 7,2015
Hivi umewahi kujiuliza inakuwaje inakuwa rahisi kwa mke kumsubiri mume
wake hata kama anachelewa kwa jinsi gani, hapa namaanisha labda
unamsubiri muende sehemu, au unamsubiri ukiwa kwenye gari na yeye
akifanya kitu fulani au kuongea na mtu flani au ametoka kwenda kununua
kitu flani, na mara anaporudi anaweza hata asiombe msamaha au kueleza
kilichomchelewesha na bado mke wake anaweza hata asiulize au kumaind,
akaichukulia poa tu au hata akiuliza sio kwa kukomaaa sanaaaa, lakini
sasa ngoja mke amcheleweshe au kumsubirisha mume wake dakika tano,
Duuuuuuuuh!!!! hayo matusi, hayo maneno, huo mnuno, huko kuzira, huko
kuuchuna na visasi visivyokuwa na mpango utadhani anaushemeji na
ibilisi.
Hivi kwanini ukipumua wewe havinuki au vinanukia na wakipumua wengine ndio janga la kitaifa?? Ukimuudhi mwingine anyamaze, akikuudhi yeye ni shiiidaaaaa!! Acha hizoo banaaa.
Hivi kwanini ukipumua wewe havinuki au vinanukia na wakipumua wengine ndio janga la kitaifa?? Ukimuudhi mwingine anyamaze, akikuudhi yeye ni shiiidaaaaa!! Acha hizoo banaaa.