KAMA HAKUNA MSAHAMA,HAKUNA MAPENZI
Umesikia kwenye matangazo mengine ya biashara wanasema “kama unampenda
utamlinda”, lakini labda na mimi nikwambie kitu kingine cha muhimu na
kilicho halisi kwamba “Kama unampenda, utamsamehe”. Kama bado mpenzi
wako anaona ugumu sana kukusamehe basi fahamu kwamba unanafasi ndogo
sana kwenye moyo wake. Upo uhusiano mkubwa sana kati ya kupenda na
kusamehe, vitu hivi viwili vinaoana sana na ni ngumu kuvitofautisha, ni
alama iliyowazi kabisa kwamba ukiona kusamehe kunaugumu baina yenu basi
penzi lenu nalo linashida. Hapa sizungumzii yale makosa ya
kurudiwarudiwa mara kwa mara na ile tabia ya kuomba radhi pasipo
kumaanisha. Always kumbuka “No forgiveness, no love” – Chris Mauki