Bukobawadau

KIJANA SALUM KABAJU ATEMBELEA WAGONJWA NA KUTOA MSAADA KATIKA HOSPITALI YA MKOA

Mdau Salum Kabaju pichani katikati akiwa ameongozana na mama yake mzazi Bi Samia Rajabu mkazi wa Kashabo Mjini Bukoba wameweza kuwatembelea na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Mkoa wa Kagera.
 Katika tukio hili ambalo ni mfano wa kuiga wakiwa wamesindikizwa na ndugu wa karibu wametembelea na kusalimia Wodi ya watoto , Wodi ya wazazi na kuwakumbuka wagonjwa wengine wasiojiweza kwa kuwapa misaada mbalimbali ambayo itawafariji na kuwasaidia katika maisha yao.
 Bi Samia Rajabu akimfariji mmoja wa wagonjwa na kumkabidhi msaada wake.
 Aidha wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo wametoa shukrani zao za dhati kwa wadau kufuatia kitendo cha kuwakumbuka na kuwatembelea kuwafariji.
“Tumepata faraja kubwa sana kwani kwa kawaida anapokuja kukuona mtu ambaye hamfahamu na kukupa pole unafarijika kwa kuwa ni kitu ambacho hukukitegemea”, walisema wagonjwa hao.
Kijana Salum akiwa ameongozana na ndugu wa karibu wametoa vitu mbalimbali kama Sukari,sabuni za kufulia na kuogea, Mafuta ya kujipaka ,miswaki na dawa za meno ambavyo wamevikabidhi kwawagonjwa waliokuwa wamelazwa katika wodi za wazazi, wanawake na watoto .
 Bi Shamila akiendelea kuwafariji wagonjwa waliolazwa wodi ya Watoto katika Hospitali ya Mkoa
 Mama anayemuuguza mtoto wake mwenye matatizo ya kifua kikuu.
 Mtoto mgonjwa anayesumbuliwa na Kifua kikuu akiwa anaendelea vizuri na matibabu.
 Zoezi la kuwazungukia  na kuwafariji wagonjwa likiendelea
 Mmoja wa wagonjwa  anayesumbuliwa na Malaria
Katika kutoa misaada mbalimbali wadi ya wazazi kutoka kitanda kimoja hadi kingine
Muonekano wa nje ya Wadi ya wanawake.
Mdau akikabidhi msaada kwa wanawake waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Kagera

 Kijana Salum Kabaju na Mama yake Mzazi Bi Bi Samia Rajabu.
 Beatrice Kambuga matroni wa Hospitali ya Mkoa Kagera akiongea na BUKOBAWADAU amesema kuwa taratibu za kwenda kuwatembelea wagonjwa na kutoa msaada hospitalini hapo ni kuandika barua ya maombi utawala ukishakubaliwa unapangiwa siku nzuri yenye nafasi.
 Kushoto ni Afisa mhuguzi Hospitiali ya Mkoa Bi Alfonsina Mgarula na matroni  Bi Beatrice wakijadiliana Afisa lishe wa hospitali ya Mkoa Bi Cecilia Mtega pichani kulia
 Mgonjwa huyo pichani hana uwezo wowote ,hana mshirika wala msaidizi,anahitaji msaada zaidi.
Kijana Salum akimsikiliza Mgonjwa ambaye anahitaji msaada zaidi kwani ametengwa na jamii, kwa jina  anayejulikana kama Prakiseda Joseph mwenyeji wa Karagwe 
 Matukio mbalimbali yakiendelea
Bi Christa mtumishi wa hospitali ya Mkoa Kagera
 Ubao wa matangazo uliopo sehemu ya mapokezi wodi ya Wanawake
Taswira hali ya wagonjwa hospitalini
Utaratibu wa kutoa msaada ukiendelea
 Kwa matukio ya picha zaidi ya 100 tembelea ukurasa wetu wa facebook kwa kubofya hapa >>Bukobawadau Entertainment Media
 Akiwafariji baadhi ya watoto hospitalini hapo
 Mdau Salum akiendelea kuwafariji wagonjwa
  Bukobawadau tunatoa wito kwa taasisi Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali ,watu binafsi na mashirika ya umma wawapatie msaada wagonjwa mahospitali pindi watakapopata nafasi.
 Afisa mhuguzi Hospitiali ya Mkoa Bi Alfonsina Mgarula
 Matroni Bi Beatrice akitoa shukrani zake kwa Mdau Salum Kabaju
 Mwisho Bukobawadau Blog tunawaomba watu wote wenye mapenzi mema kuwasaidia wagonjwa wenye kuhitaji  na kuwafariji
BOFYA HAPA >>Bukobawadau Entertainment Media kujiunga katika ukurasa wetu wa facebook  kwa matukio ya picha zaidi,tafadhari 'like' ukurasa huo kwa habari na matukio ya papo hapo!!


Next Post Previous Post
Bukobawadau